ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 24, 2018

MBUNGE WA KWIMBA HAONI HASARA KUMEGA SEHEMU YA MSHAHARA WAKE KUKARABATI BARABARA ZA JIMBO LAKE



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Moja kati ya changamoto zinazorudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwa vijiji vingi nchini Tanzania ni ubovu wa miundombinu ya barabara.


Pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya 5 yenye kasi, bado barabara nyingi za maeneo hayo zinapitika kwa shida na hata kusababisha baadhi ya vyombo vya usafiri kukongoroka au kuharibika kabisa na nyakati nyingine hasa kipindi cha masika barabara hizo kutopitika kabisa kiasi kinachosababisha baadhi ya watoa huduma za usafiri na usafirishaji kulazimika kutoza nauli mara 5 au 10 zaidi ya tofauti ukilinganisha na gharama ya kusafiria umbali huo huo maeneo ya mijini (kwenye barabara za lami).

Gharama kubwa za usafiri na usafirishaji siyo tu inachangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi kiuchumi na biashara, bali pia yanafifisha juhudi za Serikali kupambana na umasikini kwa wananchi kwani imekuwa ikichangia baadhi ya vifo vya akinamama, watoto na wagonjwa ambao wangehitaji rufaa au huduma katika hospitali kubwa zilizoko mijini lakini wameshindwa kutokana na kushindwa kumudu gharama usafiri.

Kutokana na changamoto hizo za ubovu wa barabara kwa vijiji vya jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Mhe.SHANIF MANSOOR, ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amefanya ziara ya kukagua kujionea hatua zilizofikiwa za ukarabati wa barabara zilizo kwenye mradi. 

Mbunge huyo, amekagua barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 6, inayotoka kijiji cha Mwashigi kata ya Nyamilama kuelekea kata ya Mwakilyambiti ambayo amesema  ikikamilika itachochea maendeleo na urahisishaji wa utoaji huduma kwani inaunganisha vijiji mbalimbali vya jimbo la Kwimba.

Aidha mbunge huyo wa vitendo, amesema amehamasika kuikarabati barabara hiyo kutokana na adha ya muda mrefu aliyoiona kwa wapiga kura wake sanjari na kutimiza ahadi aliyoitoa kipindi cha uchaguzi. "Itambulike kwamba ukarabati huu fedha zake si za mfuko wa jimbo bali ni kutoka kwenye mshahara wangu, najitolea kwa moyo wa dhati kwa kuwa nami ni mwananchi wa hapa na ninaogopa kuulizwa juu ya ahadi yangu niliyoitoa" Alisema MANSOOR. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.