NaibuWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa tofali linalotengenezwa na wafungwaikiwa ni mpango wa uongozi wa gereza la Kwamngumi kukabiliana na changamoto ya makazi kwa askari, Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo,Christopher Mwenda, lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa nyumba
iliyojengwa na matofali
yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamngumi lililopo Wilayani
Korogwe, mkoani Tanga.Kushoto ni Mkuu wa
Gereza hilo, Christopher Mwenda.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia tofali ambazo
zimetengenezwa na wafungwa wa Gereza la Kwamngumi, ambazo hutumika kujengea
nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika
shughuli za uzalishaji na kilimo.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa Kaunda suti), na ujumbe alioongozana
nao wakipita mbele ya nyumba iliyojengwa
kwa kutumia matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamgumi
lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Magereza
kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli
Na Mwandishi Wetu.
Serikali imeteua jumla
ya magereza kumi nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli la kulitaka Jeshi la Magereza litumie
rasilimali watu ya wafungwa kuzalisha mazao kwa ajili ya biashara na chakula
badala ya serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa.
Akizungumza wakati wa
ziara ya kukagua utekelezaji wa agizo hilo katika Gereza la Kwamngumi wilayani
Korogwe ,mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni alisema utekelezaji huo unaenda sambamba na uteuzi wa magereza kumi ya
kilimo nchini na akiweka wazi uwapo wa mpango maalumu wa kutathmini na kupima
mpango mkakati huo kwa kila gereza.
Aliyataja magereza hayo
kuwa ni Songwe(Mbeya),Kitai(Ruvuma),Ludewa(Njombe), Mollo (Rukwa), Kitengule
(Kagera) ambayo yameteuliwa kulima mahindi, mengine ni Idete na Kiberege
(Morogoro) yaliyoteuliwa kulima mpunga huku Kitete (Rukwa), Kitengule (Kagera)
na Gereza la Arusha yakiteuliwa kulima maharagae
“Tunahitaji matumizi
sahihi ya rasilimali watu na ardhi tuliyonayo katika magereza yetu itumike
ipasavyo kwa shughuli za uzalishaji ili tuweze kutekeleza amri ya Mheshimiwa
Rais, huku lengo la wizara kupitia jeshi la magereza ni kuweza kuwekekeza fedha
kwa kulitumia shirika la uzalishaji mali lililopo ndani ya jeshi hilo na
ikiwezekana hapo baadae tuweze kutafuta wateja watakaonunua mazao
yatakayozalishwa katika mashamba hayo,” alisema Masauni.
Akizungumza katika
ziara hiyo, Mkuu wa Gereza la Kwangumi, Christopher Mwenda, alisema wao kama
uongozi wa gereza hilo wamejipanga vizuri katika utekelezaji wa aguzo hilo huku
akiiomba wizara kuongeza vifaa vya kilimo ili waweze kuzalisha kwa kiwango
kikubwa zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.