Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akilitaka shirika la SIDO kuwasaidia wajasiriamali wa mkoa wa Tabora kutengeneza mashine za kisasa zitakazowasaidia kukausha bidhaa zao za chakula kisasa na kuziongezea thamani alipokuwa akifunga Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji ambalo limefanyika mkoani hapo kwa siku tatu leo,kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda (kulia) akizitaka taasisi zilizipo chini ya wizara yake kujipanga kukutana na uongozi wa mkoa wa Tabora kwa ajili ya kushauriana namna ya kufanikisha maadhimio ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji leo wakati kufunga jukwaa hilo mkoani hapo,kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Magreth Sitta akitoa shukrani kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa niaba ya wabunge wenzake kufanikisha Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji wakati wa ufungaji wa Jukwaa hilo liloendeshwa mkoani hapo kwa siku tatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi akiiomba serikali kutafuta Mwekezaji atakaye uendeleza na kuuboresha uwanja wa Michezo wa Ali Hassan Mwinyi uliyopo Tabora Mjini na kuwasaidia leo wakati wa kufungwa kwa Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoa hapo.
Kaimu Mhariri Mtendaji Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Bibi.Tuma Abbdalah akipongeza mwitiko wa wakazi wa Tabora katika kushiriki Jukwaa la fursa za Biasharana Uwekezaji na hamasa ya maendeleo waliyoonyesha wakati wa kufungwa kwake leo mkoa hapo.
Mkuu wa Mkoa
waTabora Mhe.Aggrey Mwanri akimweleza Mwenyekiti wa Jukwaa la Fursa za Biashara
na Uwekezaji namna Mkoa huo umejipanga kuleta mabadiliko baada ya kumalizika
kwa Jukwaa hilo mkoani leo wakati wa
kufungaji Jukwaa hilo.
Na Anitha Jonas –
WHUSM
24/11/2018
TABORA
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe ameitaka taasisi ya SIDO
nchini kuonyesha weledi wake kwa kuwa tengenezea wajasiriamali wa Mkoa wa Tabora kifaa chenye
Teknolojia rahisi ya kukaushia bidhaa zao za chakula ili kuziongezea ubora.
Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema
hayo leo Mkoani Tabora alipokuwa
akifunga Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji lililokuwa likifanyika
Mkoani hapo kwa siku tatu kwa lengo la
kutangaza fursa za biashara na uwekezaji za mkoa huo pamoja na kuwajengea uwezo
wajasiriamali wa kuboresha bidhaa zao
pamoja na kuona umuhimu wa rasimisha bidhaa hizo kwa ajili ya kuongeza wigo wa
biashara na kipato.
“Naupongeza uongozi
wa Mkoa huu kwa hatua waliyochukua kufikia maadhimio ya kugawana majukumu ya
kuendeleza sekta ya viwanda
kimkakati kwa kuhakikisha kila wilaya
inawajibika kuleta maendeleo kwa wananchi wake pamoja na Halmashauri ya Mji wa
Tabora kutekeleza utengaji wa eneo la uwekezaji
kwa ajili ya maendeleo ya viwanda hakika jukwaa hili limesaidia kutia
chachu ya mafanikio katika mkoa huu,”alisema Mhe.Mwakyembe.
Naye Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda aliwasihii waandaaji wa Jukwaa
hilo ambao ni Kampuni ya Magazeti Tanzania (TSN) kuhakikisha wanatembelea Mikoa
yote nchini na baada ya hapo kushuka katika ngazi ya Wilaya kama alivyoagiza
Mhe.Waziri Mkuu Kassim Majiliwa katika ufunguzi wa Jukwaa hilo.
“Kwa kuzingatia manufaa
ya Jukwaa hili nimeziagiza taasisi
zilizopo chini ya Wizara yangu kujipanga na kuja hapa Tabora na kuzungumza
na viongozi wa Mkoa huu pamoja na kutoa ushauri
wa kitaalamu ili kufanikisha maadhimio ya Jukwaa hili kwa manufaa ya
taifa,”alisema Mhe.Kakunda.
Kwa upande Kaimu
Mhariri Mtendaji (TSN) Bibi.Tuma Abdallah aliupongeza uongozi wa Mkoa huo
pamoja na kuwashukuru Mawaziri waliyoshiriki Jukwaa hilo kwa uwepo kwani uwepo
wao umesaidia kufanikisha jukwaa hilo na kulifanya kuwa la kihistoria kwa
mikakati iliyowekwa ili kufanikisha utekelezaji wa maadhimio yake.
“Katika Jukwaa hili la
nane tangu tumeanza uendeshwaji wa Jukwaa hili nimejifunza kuwa
Tabora ina hari ya hali ya juu ya kupata maendeleo kwa namna walivyojikita
katika mijadala na hoja mbalimbali wanazo ziibua hii yote inaonyesha kiu kubwa
ya wananchi wa Mkoa huu kutaka kupata maendeleo”alisema Bibi.Tuma.
Pamoja na hayo nae
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri alisisitiza kuwa uongozi wa mkoa
hautakubali ujio wa Jukwaa hilo
kutowaletea manufaa kwani kwa maadhimio ya jukwaa hilo wamejipanga vizuri kuhakikisha kila Wilaya inatekeza mradi ambao utaleta
manufaa kwa wananchi wake kwa kutelekeza hilo Wilaya ya Urambo itajenga Kiwanda cha Tumbaku,Wilaya ya Kaliua itaandaa
ranchi pamoja kiwanda cha alizeti na
karanga halikadhalika uuzaji wa mazao ya misitu kwa kuzingatia sheria,Wilaya ya
Uyui itasimamia masoko ya Kilimo na Mifugo na Wilaya ya Nzega kuanzisha Kiwanda
cha uchakataji wa Nyama na Ngozi pamoja na kuanzisha ranchi pamoja na Wilaya ya
Igunga kutekeleza kilimo cha Mpunga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.