Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya NaibuWaziri kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoaniTanga . Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo na Kulia niKatibu Tawala wa Wilaya hiyo, Warda Abeid. Picha na Wizara ya Mambo yaNdani ya Nchi
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo akizungumza katika kikao chandani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilayaya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) kukagua shughuli za ulinzi nausalama wilayani Kilindi mkoani Tanga . Kulia ni Katibu Tawala wa Wilayahiyo, Warda Abeid. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi , EdwardBukombe, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe waKamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikaziya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani, ) kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindimkoani Tanga . Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Serikali imedhamiria kujenga Vituo vya Polisi 65 katika wilaya mbalimbali nchiniikiwa ni juhudi za kukabiliana na uchakavu na upungufu wa vituo vya polisinchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, MhandisiHamad Masauni baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Polisi cha Songeambacho ndio kituo kikuu katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga
Alisema Serikali inatambua changamoto za vituo vya polisi ikiwemo uchakavu,udogo wa majengo katika vituo mbalimbali nchini na iko katika mpango wakujenga vituo vya polisi 65 ili kuwepo na ulinzi thabiti wa raia na mali zao.
“Serikali inatambua changamoto ya vituo vya polisi hasa katika wilaya mpyanchini, ikiwepo uchakavu wa majengo, kwahiyo uko mkakati maalumu wa kujengavituo vya polisi 65 nchi nzima ili kuweza kukabiliana na matukio ya kiuhalifu,lengo la serikali ni kuhakikisha raia wake na mali zao zinakua salama na matukioya kiuhalifu yanapungua na kutoweka kabisa,” alisema Masauni
Alisema Serikali pia inakaribisha nguvu za wananchi na wadau mbalimbali ambaowako tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi huku akipongeza baadhi ya maeneonchini ambako vituo vya polisi vimejengwa kwa ushirikiano wa michango yawananchi na serikali.
Awali akitoa taarifa ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi, Mkuu wa Wilayaya Kilindi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Sauda Mtondooalisema hali ya uhalifu kuanzia kipindi cha Januari hadi Oktoba 2018 ilikua yawastani huku kukiripotiwa upungufu wa makosa kwa asilimia 9.8 kati ya mwaka2018 na 2017.
“Kwa mujibu wa takwimu za uhalifu kulikuwa na jumla ya makosa makubwa yajinai 163 ndani ya mwaka huu yaliyoripotiwa kwa kulinganisha na makosa 179yaliyoripotiwa ndani ya mwaka 2017, ukiwepo upungufu wa makosa 16 katikavipindi hivyo viwili,” alisema Sauda
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mbunge wa Kilindi, Omari Kibuaalimshukuru Naibu Waziri kwa kufika jimboni hapo kujionea hali halisi ya kituohicho kikuu cha wilaya baada ya kumuomba kufanya hivyo wakati wa kikaocha bunge kilichomalizika hivi karibuni
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.