Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoani Njombe Kimetangaza kuchukua hatua na Kumburuza Mahakamani Aliyekuwa Mgombea Wao wa Udiwani Katika Uchaguzi Mdogo wa madiwani Kata ya Itulahumba Wilayani Wanging'ombe Baada ya Kujitoa katika hatua za mwisho za kinyang'anyilo hicho cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika AUGOST 12 mwaka huu.
Mgombea Huyo wa udiwani Bwana Samwel Kihombo Awali Aliwekewa Pingamizi na Chama Tawala Lakini Akashinda Rufaa na Kuwa Mgombea Pekee Kwa Upande wa Vyama Vya Upinzani Baada ya Mgombea wa CHADEMA Kuondolewa Baada ya Kuwekewa Pingamizi na Chama Tawala.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.