Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Dk.Hery Mwandolewa akiwa ofisini kwake Heameda Medical Clinc Bunju B jijini Dar es Salaam.
* Madaktari Bingwa nchini waungana na wezao kutoka India kuwahudumia wananchi,waombwa kujitokeza kwa wingi
Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii
HEAMEDA Medical Clinic iliyopo Bunju B njia ya kuelekea Mabwepande imetangaza kambi ya uchunguzi wa afya ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wote na kwamba hakutakuwa na gharama.
Akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Dk. Hery Mwandolela amesema wameaza kambi hiyo ya uchunguzi leo jijini Dar es Salaam kwa kupima wananchi mbalimbali waliojitokeza na kusisitiza upimaji huo ambao umeanza leo Julai 26 utaendelea hadi Julai 28 mwaka huu.
Amesema upimaji huo unafanywa na Madaktari bingwa wa hapa nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka nchini India na lengo kuu ni kuwawezesha wananchi kutambua afya zao mapema na iwapo watabainika kuwa na tatizo la kiafya waaze tiba mapema.
Amefafanua huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ya uchunguzi ni pamoja na kupima magonjwa yasiyoambukizwa yakiwemo ya Moyo ,sukari,shinikizo la damu,Tenzi Dume, lehemu(cholestrol) nakiwango cha mafuta mwilini."Madaktari bingwa wa Heameda Medical Clinic kwa kushirikiana na madaktari bingwa wengine nchini pamoja na madaktari bingwa kutoka India tutatoa huduma hizo kwa kiwango cha hali ya juu.
Nakuongeza kuwa " hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi nakwamba huduma hii inafanyika kwa siku tatu ambapo tumeaza leo na tunaendelea kesho na keshokutwa na hakuna gharama yeyote ."amesema Dkt Mwandolela.Amesisitiza kwakutambua umuhimu wa afya yako wameamua kufanya kampeni hiyo ya kupima magonjwa hayo wakiamini ni fursa ya kila mwananchi kujitambua kiafya mapema..
Katika kampeni hiyo kwa siku ya leo ambayo ni ya kwaza idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza lakini Dkt.Mwandolela anafafanua kwa idadi ya madaktari bingwa waliopo nivema wananchi wakaendelea kujitokeza kwani wote watahudumiwa kwakupata vipimo vya afya zao.
Muonekano wa sehemu ya mapokezi ndani ya Clinic hiyo
Muonekano wa moja ya chumba chenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa/matibabu
Muoneakano wa Clinic hiyo kwa nje
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.