Kituo kimoja cha utafiti nchini Marekani kimefichua kuwa serikali ya zamani ya nchi hiyo ilikuwa ikilifadhili kifedha tawi la kundi la kigaidi la al Qaida huko Sudan.
Kituo hicho cha utafiti kwa jina la Middle East Forum kimefichua na kueleza kuwa serikali ya Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama ilipasisha kiasi cha dola laki mbili kama msaada kwa moja ya matawi ya mtandao wa kigaidi wa al Qaida huko Sudan kwa jina la Taasisi ya Kiislamu ya Misaada.
Msaada huo wa fedha uliidhinishwa huku Wizara ya Fedha ya Marekani ilikuwa ikifahamu kuwa tawi hilo lipo katika orodha ya makundi ya yanayowafadhili kifedha magaidi. Pamoja na hayo yote, ushadhi mpya unaonyesha kuwa ofisi ya kudhibiti fedha za kigeni katika Wizara ya Fedha ya Marekani tarehe 7 Mei mwaka 2015 ilitoa kibali cha kupatiwa fedha kundi moja lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida huko Sudan. Kundi hilo lilikuwa na nafasi katika kutoroka Usama bin Laden katika miaka baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.