ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 26, 2018

TUTEGEMEE NINI TOKA KWA MA-BLOGGERS WANAOKUTANA MJINI MOROGORO HII LEO



GSENGOtV


Taasisi ya Freedom House kupitia mradi wake wa Data Driven Advocacy imeandaa mafunzo kuhusu Altenative Media kwaajili ya waandishi wa habari unaofanyakazi kupitia mfumo wa mitandao shughuli inayofanyika mjini Morogoro.


Zaidi ya waandishi 25 wamekutana hapa.


Nini tutegemee toka kwao?



HASARA 5 ZA MITANDAO YA KIJAMII
Mitandao ya Kijamii imekua kwa kasi ya ajabu sana kuanzia mwaka 2006 mpaka leo tofauti ni kubwa sana. Kuanzia Facebook, twitter, Instagram mpaka Youtube zimekuwa kwa kasi ya ajabu na kukusanya mamilioni ya watumiaji.
Kila kitu kina faida na hasara pia naweza kusema kuwa mitandao ya kijamii ina athari kubwa sana katika jamii, pia imeweza kurahisisha mambo mengi sana katika jamii yetu inategemea na mtumiaji anayetumia.
Zifuatazo ni baadhi ya Hasara za kutumia mitandao ya kijamii:
1. Kuvunjika kwa Maadili yetu
Mitandao ya kijamii kama yalivyo maendeleo yoyote yameletwa na watu wa Magharibi, hivyo hasa kwa nchi zetu za Afrika zimeonja utandawazi wa hali ya juu ila sisi waafrika tuna mila na desturi zetu ambazo ziko tofauti na wazungu baadhi ya vitu vilivyoharibu maadili yetu ni ukiingia kwenye mtandao wowote wa kijamii utakutana na matusi yaliyopitiliza yaani lugha ambayo watu wanatumia utakimbia. Pia vijana kufuata wanayofanya wazungu na kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, kupiga picha za uchi n.k.
2. Majanga Kama Vifo
Kupitia mitandao ya kijamii hasa facebook au Instagram watu wanakutana wanachat lakini hawajuani wanahis mtu unayeongea naye ni mtu mzuri kuja kuonana wengi wanaishia kuuliwa au kubakwa. Kuna stori niliisikia hapa hapa Tanzania msichana kakutana na mvulana facebook wakapendana ingawa hawajawahi kuonana siku wakasema wakutane Magomeni, yule msichana hakuonekana tena wamekuja kukuta maiti yake Bagamoyo.
3. Wizi na Utapeli
Kwa bahati mbaya mitandao ya kijamii inatumika vibaya sana tofauti na lengo au sababu zilizowekwa kuna watu wanatumia mitandao ya kijamii kuibia wengine yaani utapeli kwa kuuza vitu feki  na kadhalika.
4. Uzembe
Mitandao ya kijamii imesababisha uzembe na kujiendekeza kwa watu wengi hasa vijana wenye nguvu kabisa. Yaani hivi sasa kuna watu ambao watashinda kutoka asubuhi mpaka jioni kwenye facebook au instagram bila kufanya kazi yoyote yaani myu ataamka asubuhi kabla hata ya kufanya kiyu chochote aingie kwanza kwenye mitandao ya kijamii ndo asikie raha kitu ambacho hakileti maendelea yoyote.
5. Kuvunjika kwa Mahusiano 
Kwa kiasi kikubwa mitandao ya kijamii imepelekea kwa mahusiano mengi sana kuvunjika yaani watu wengi wanaitumia vibaya hii mitandao, zamani ilikuwa ili upate mchepuko basi ukakutane mtu mbali huko lakini siku hizi unakutana na mtu kwenye kiganja cha mkono wako hivyo imerahisisha zaidi watu kupata michepuko na kuvunjika kwa mahusiano mengi sana, hasa hawa wasichana wanaopiga picha za nusu uchi watu wanajikuta wanaharibu mahusiano
Ingawa Mitandao ya Kijamii ina faida nyingi hizi ni baadhi tu ya hasara za kuwepo kwa mitandao ya kijamii hasa kwa hizi nchi zetu za Afrika.

Je kuna hasara nyingine ambazo sijazitaja tafadhali funguka hapo chini na uongezee za kwako......
KAA TAYARI KWA KUZIJUA FAIDA.
Kutoka kushoto ni Exaud Mtei wa Habari 24 Blog akifuatiwa na Marco Maduhu wa Shinyanga News Blog.
Kutoka kushoto ni Given Mashishanga wa Global Tv Online, James Range, Midraj Ibrahim wa Mwananchi Comunications.

Kutoka kulia ni John Bukuku wa Full Shangwe Blog.
Kutoka kushoto Eliya Mbonea kutoka Mtanzania Digital,
Mbele pichani ni George Binagi wa BMG Habari
Kutoka kushoto ni Pamela Mollel wa Jamii Blog, Malunde Blog na Full Shangwe Blog.
'Muosha huoshwa'

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.