ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 26, 2018

KAMPUNI ZA HOWDEN BROKING NA B.R,PURI ZAJA NA MKAKATI WA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA


David Howden, Afisa Mtendaji Mkuu wa Hyperion and Howden amesema (Pichani) “Hii ni hatua nzuri kwetu kwa kampuni ya Howden kuwa na mshirika wa kibiashara barani Africa na tunayo furaha kushirikiana kibiashara na kampuni ya B.R. Puri, ikiwa ni moja ya kampuni kubwa inayoongoza katika soko la Tanzania.  Mikakati yake mikubwa ya kibiashara inaenda sambamba na mikakati ya Howden na tuna imani kwa kuunganisha mikakati yetu ya kibiashara kupitia kampuni mpya ya Howden Puri tutaweza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na jumuiya za kimataifa nchini Tanzania, Afrika Mashariki na zaidi ya hapo.  Kupitia ushirikiano huu tunaona zipo fursa nyingi zinazotuwezesha kukua zaidi kibiashara”

Akiongelea ushirikiano huu wa kibiashara, Arun Puri, Mwenyekiti wa Howden Puri alisema “Kampuni ya BR Puri & Company, ilianzishwa na baba yangu kwenye miaka ya 1950, ikiwa ni moja ya kampuni ya kwanza nchini Tanzania kujishughulisha na biashara za uwakala wa bima. Naamini kwa kuunganisha ujuzi wetu na uzoefu mkubwa tulionao na utaalamu wa Howden wa kutoa huduma katika nchi nyingi duniani kutanufaisha wateja wetu tulio nao na watakaojiunga nasi.

Umesh Puri, Afisa Mtendaji Mkuu wa Howden Puri, aliongeza kusema “Tukiwa kampuni ya uwakala wa bima inayoangalia mbele hapa nchini Tanzania, lengo letu ni kubuni huduma mpya za bima zinazoendana na hali ya soko la Tanzania. Howden imechagua kushirikiana na kampuni ya Tanzania kibiashara ikiwa ni ya kwanza barani Afrika kutokana na jitihada nzuri zinazofanywa na wasimamiaji wa sekta ya bima kuiboresha zaidi sambamba na mazingira mazuri ya kufanyia biashara yaliyopo nchini kwa ujumla”.

*Biashara zake nchini kuendeshwa kwa jina la Howden Puri Insurance Brokers Limited

Kampuni ya kimataifa ya Howden, chini ya kampuni mama ya Hyperion Insurance Group imeingia katika ushirikiano wa kimkakati wa kukuza biashara na kampuni kongwe ya masuala ya bima nchini ya B.R. Puri & Company Limited, ambapo chini ya ushirikiano huo imeanzishwa kampuni itakayoendesha biashara zake nchini inayojulikana kwa jina la Howden Puri Insurance Brokers Limited.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.