Kikundi cha watu wanaotoka mikoa ya kusini ambao wanaishi jijini Mwanza maarufu kama MBEYA NI KWETU mwishoni mwa wiki wamefanya harambee ya kukusanya fedha ambazo zitatumika kujenga chuo cha ufundi kitakachotoa elimu kwa vijana waliohitimu elimu ya msingi na wamekosa alama za ufaulu wa kuendelea na elimu ya sekondari.
Akisoma lisala kwa mgeni ramsi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk Philis Nyimbi aliyemwakilisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Akson Mwansasu, katibu wa kikundi hicho Paul Mwaiteleke amesema kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka 2018, hadi kufikia sasa kina jumla ya wanachama 102 na fedha zilizopo benki kutokana na michango ni millioni 30,208,348/=
Akiongoza harambee hiyo ambayo ilidhamiria kukusanya shilingi kiasi cha Shilingi milioni 20 na hatimaye kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni saba, Dk Nyimbi amewapongeza na kuwataka kuendelea na juhudi za kukusanya fedha ili kuweza kutimiza adhma waliyojiwekea.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.