Dar es Salaam. Rais John Magufuli, leo (Alhamisi) amefanya uteuzi wa mabalozi watano watakaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema mabalozi hao wataapishwa kesho (Ijumaa) Ikulu jijini hapa.
Mabalozi hao ni Emmanuel John Nchimbi ambaye ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Brazil, Mbelwa Brighton Kairuki ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania, China, George Kahema Madafa ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Rome , Italy.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Muhidin Mboweto kuwa balozi.
Tarehe ya kuapishwa na kituo cha kazi cha Mboweto vitatangazwa baadaye.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.