ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 14, 2012

QUESTION CREW ndio kinara wa serengeti dance la fiesta 2012 mkoani tanga

Mmoja wa waratibu na jaji,Isakwisa Thomson akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi kinara la Questions Crew kati ya saba yaliyojitokeza kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,lililofanyika jioni ya leo ndani ya kiota cha mangoma cha Lakasachika mkoani Tanga.
Mmoja wa waratibu na jaji,Isakwisa Thomson akiwa na kitita cha fedha taslim sh milioni moja,kwa ajili ya kukabidhi kwa kundi la Questions Crew lililoibuka mshindi wa kwanza kati ya makundi saba yaliyojitokeza kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,lililofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Lakasachika mkoani Tanga.
Baadhi ya wacheza shoo wa kundi la Questions Crew wakizungumza machache mara baada ya kukabidhiwa kitita chao cha shilingi milioni moja
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti-Tanga wakikabidhi Kreti moja ya bia ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa kundi la Questions Crew mara baada ya kuibuka washindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012 mkoani Tanga.
Watu mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.
Kundi la Sweet Girls likionesha umahiri wake kucheza kwenye shindano la kulisaka kundi kinara la Serengeti dance la Fiesta 2012
Kundi la la Street Colour likionesha umahiri wa kucheza mbele ya sehemu ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza jioni ya leo kushuhudia shindano la Serengeti dance la Fiesta lililofanyika ndani ya ukumbi wa Lakasachika
Kundi la Questions Crew likicheza kouwania kitita cha milioni moja kilichotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti sambamba na kreti moja ya bia.
Mdau Thomson akikata kiu yake safi kabisaa.
Palikuwa hapatoshi leo ndani ya ukumbi wa Lakasachika.
Macho mbeeeeele...
Pichani juu na chini Sehemu ya wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga waliojitokeza kushuhudia shindano hilo lilovuta hisia za vijana wengi
Mmoja wa majaji wa shindano hilo B Dozen akifafanua jambo wakati wa kumsaka kinara wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tanga.
Maujuzi na maufundi..


Mmoja wa majaji wa shindano hilo Isakwisa Thomson akifafanua jambo wakati wa kumsaka kinara wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tanga.

Majaji wa shindano la Serengeti dance la fiesta 2012 wakijadiliana jambo wakati shindano likiendelea ndani ya ukumbi wa Lakasachika jioni ya leo,ambapo wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga walijitokeza kwa wingi na kujionea vipaji

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.