ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 24, 2012

MARAIS WASTAAFU NANE WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA NCHINI AFRIKA KUSINI KWA SIKU TATU.








                                              Pichani shoto ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,mapema leo jioni,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini.Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na mwisho ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo.


                                                                  Pichani kulia ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo akifafanua jambo kwa makini wakati wa mchakato wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ulipokuwa umepamba moto jioni ya leo,katika mkutano uliofanyika kweny moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo mchana,Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na   Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa
                                                                              Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
                                                                           Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
                                                                                                                                                   Pichani juu na chini Mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ukiendelea ndani ya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo mchana.

                                                                                                                                                   Baadhi ya Marais Wastaafu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa kwenye mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
                                                                                                                                                    Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,ambaye pia ni Mratibu mkuu wa mkutano akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Mkutano huo mapema leo mchana.
                                                                                                                                           Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin,Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar,Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Rais Thambo Mbeki wa Afrika Kusini,Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria,Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Rais Rupiah Banda wa Zambia wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo mchana kabla ya kuanza mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
                                                                                             Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akijadiliana jambo na Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin walipokuwa wakiwasili kwenye viunga vya vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

Pichani  mbele ni Marais Wastaafu wa Tanzania,Ally Hassan Mwinyi na  Benjamin Mkapa sambamba  na  Marais wengine wakiwasili katika viwanja vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
                                                                                                    Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka nchini Tanzania,wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kuripoti mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.Shoto ni Yvonne Msemembo (ITV) ,Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper),Nestor Mapund,Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications), Muondosha Mfanga (The Guardian) pamoja na Deus Mjatta (ITV).
                                                                                                    Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakijadiliana jambo nje ya ukumbi,kabla ya kuanza kwa Mkutano huo,Shoto ni Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications),Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper), Muondosha Mfanga (The Guardian).
                                                                                      Baadhi ya wanafunzi kutoka vyo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,ambao umewashirikisha Marais Wastaafu nane wa Afrika. 
========  ====== ========
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wakutana nchini Afrika Kusini.
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wamekutana leo jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kufanya mkutano wa siku tatu ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

Marais wastaafu hao waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania, Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin, Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania, Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Rais Rupiah Banda wa Zambia.

Aidha - mbali ya Marais hao waliohudhuria mkutano huo, pia ulihudhuriwa na  Wataalam mbalimbali wa nishati, viongozi wa umma na sekta binafsi na wanafunzi na kitivo kutoka vyuo vikuu 9 vya kimataifa kikiwemo chuo kikuuu mwenyeji cha Witwatersrand a.k.a Wits. Tanzania iliwakilishwa na wanafunzi watano na walimu wawili kutoka chuo kikuu cha Dar-es-Salaam.

Mratibu mkuu wa mkutano huo - Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana juu ya ufumbuzi wa mageuzi ya nishati katika nchi za Kiafrika, na kuhakikisha nchi za Afrika zinajiwakilisha vyema katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala zima la Nishati.

Balozi Stith alisema kuwa mkutano huo utaleta mshikamano wa pamoja kwa viongozi wa sekta ya nishati na wafadhili mbalimbali wa miradi mbalimbali, ili kuhakikisha nishati hiyo inatosheleza mahitaji ya Afrika kwa ujumla. Mkutano huo wa siku 3 utafikia tamati Mei 25.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.