ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 24, 2012

MBUNGE WA ROMBO JOSEPH SELASINI APATA AJALI MBAYA WATATU WAFARIKI DUNIA

Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini amepata ajali mbaya sana wakati alipokuwa akiendesha gari lake mkoani Kilimanjaro, ambapo watu 3 kati ya watu 6 waliokuwemo kwenye gari hilo wamepoteza maisha na miili yao imechukuliwa na gari la polisi na kupelekwa hospitali ya KCMC Moshi kutoka Boma Ng'ombe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Absalom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo akielezea zaidi amesema Ilikuwa ni saa 1:00 jioni maeneo ya Boma Ng'ombe ambapo Mh Joseph Selasini wakati akiendesha gari hilo akitokea Arusha, ghafla aliona mwendesha Pikipiki wakati akijaribu kumkwepa ndipo gari lake likapinduka.

Watu wengine akiwemo mbunge huyo na mkwe wake alifahamika kwa jina la Digna Kavishe waliojeruhiwa katika ajali hiyo, wako katika hospitali ya Boma Ng'ombe hali zao zinaendelea vizuri na muda mfupi nao watapelekwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi
Chanzo: Full Shangwe

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.