ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 24, 2018

SERENGETI BOYS YAFA KIUME TAIFA.


Timu ya Uganda imefanikiwa kutinga fainali ya kufuzu Afcon u17 kwa kanda ya Africa Mashariki na kati baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Tanzania, Serengeti Boys magoli 3-1 Na sasa itacheza na Ethiopia katika fainali itakayochezwa Siku ya Jumapili August 26 saa 11:00 jioni katika dimba la Taifa Dar huku Tanzania itacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na Rwanda majira ya saa 8:00 mchana.

Tanzania tayari ana tiketi ya kushiriki michuano kama mwenyeji wa fainali za Afcon u17, 2019 zitakazofanyika Tanzania kuanzia May 12 hadi May 26 mwakani. Mshindi wa Ethiopia na Uganda atapata tiketi ya kushiriki fainali hizo kama mwakilishi kutoka Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Timu 8 kutoka katika Kanda 7 za kisoka ndio zitashiriki michuano hiyo Tanzania kama mwenyeji, Cameroon nayo imefuzu kutoka kanda ya Kati, Angola nayo imefuzu kutoka kanda ya Kusini bado kanda 5 kuwajua wawakilishi ambao wataungana na timu hizo tatu kucheza fainali ya Afrika kwa chini ya umri wa miaka 17.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.