Jean-Pierre Bemba, mmoja wa viongozi wa upinzani ambaye amezuiwa kugombea |
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameijia juu Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) kwa hatua yake ya kukata majina sita miongoni mwa majina ya waliojiandikisha kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini humo.
Kwa mujibu wa viongozi hao wa upinzani, panga hilo la kukata majina yao limesukumbwa na sababu za kisiasa tu na hivyo wametishia kwenda mahakamani kuiburuza Tume hiyo ya Uchaguzi (CENI) .
Miongoni mwa wapinzani mashuhuri ambao jinao lao limekumbwa na panga CENI, ni Jean-Pierre Bemba ambaye sasa hatoweza kushiriki kinyang'anyiro hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.