ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 26, 2018

HDIECA,NIPE FAGIO, WAKAZI WA SURVEY NA WADAU MBALIMBALI WASAFISHA BONDE LA MLALAKUWA.

Hii ndio hali halisi iliyokuwepo bonde la Mlalakuwa unaopita eneo la Survey ilivyokuwa kabla ya usafi kufanyika, kutokana na kuwa mifuko ya plastiki bado ni tatizo katika bonde la Mlalakuwa
Uchafu wa mifuko ya plastiki ikiwa imetapakaa kila kona pembezoni mwa mto na Bonde la Mlalakuwa.
Pamoja na kuwekewa onyo kali lakini baadhi ya wakazi ambao hawana mapenzi na mazingira wameendelea kutupa taka katika eneo hilo la mto na bonde.
Baadhi ya akina mama wakiwa wanaendelea kufanya usafi eneo la pembezoni mwa mto na bonde la Mlalakuwa.
Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Human Dignity Improvement and Environment Care Agency (HDIECA) Bi. Sarah Pima ambao pia ndio walioandaa zoezi la usafi katika mto wa Mlalakuwa akigawa gloves kwa wakazi ambao walishiriki usafi.
Baadhi ya wakazi wanaishi pembezoni mwa mto na bonde la Mlalakuwa wakiendelea na usafi 
Afisa Mahusiano wa Human Dignity Improvement and Environment Care Agency (HDIECA) Bi. Rabia (aliyeshika mfuko mweusi) akiendelea kukusanya taka wakati wa kufanya usafi mto Mlalakuwa 
Hii ndio hali halisi ya mto mlalakuwa 
Wakazi wa maeneo jirani na mto pamoja na bonde la Mlalakuwa pamoja na vikundi vingine vya usafi wakiendelea kukusanya taka.
 Hivi ni baadhi ya viloba vya uchafu ambao ulitolewa katika mto Mlalakuwa na maeneo ya pembezoni
Hali ilivyokuwa baada ya usafi kumalizika 
Picha zote na Fredy Njeje

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.