G.SENGO BLOG.
MADIWANI wa Jiji la Mwanza leo wamegomea kujadili
Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/2015 iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, kwa madai kuwa haijakidhi na ina ubabaishaji katika mpango mkakati wa makusanyo ya Kodi kupitia Vyanzo vyake
vya ndani.
Rasimu hiyo liyowasilishwa na Mchumi Msaidizi
Joseph Kashushula kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Jiji hilo ilionekana kuwakera sana waheshimiwa Madiwani wote bila
kujali wanatoka vyama gani vya siasa na kuanza kuchangia hoja ambazo
zimepelekea kutolewa azimio la kurudisha Kamati ya Fedha kufanyiwa marekebisha
upya na kuja na majibu ya msingi kabla ya kuwasilishwa tena na kuanza kujadiliwa.
Akizungumza wakati wa kuendesha kikao hicho Meya wa
Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula alisema kwamba kutokana na hoja za waheshimiwa
Madiwani walizochangia na kuwepo mapungufu huku Mkurugenzi na timu yake ya
wataalamu kukosa majibu ya kina kuhusiana na hoja za mpango mkakati za
ukusanyaji mapato kuonyesha kukusanya bilioni 9 tu kupitia vyanzo vyake vya
ndani.
Meya Mabula alisema kamwe hawako tayari kukaa na
kupoteza muda wa kujadili Rasimu hiyo kutokana na mapungufu hayo yaliyojitokeza
huku hoja za madiwani zikidai kuwa kupitia vyanzo vya mapato ya Halmashauri
hiyo ya Jiji vilivyopo vinaweza kukusanya kiasi cha zaidi ya bilioni 13 huku
hoja zingine zilizochangiwa ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuwa
kidogo.
“Mkurugenzi na timu yako tunaomba mrudi mkajipange
upya kwa rasimu hii hatuko tayari kukaa na kujadili haiwezekani viwanda vilivyopo
hapa Jijini vikawa vinalipa Kodi ya laki moja kwa mwaka wakati vinaingiza
mabilioni ya fedha kwa mwaka hili halikubaliki na Bajeti hii siyo rafiki kwa
mustakabali wa kuwatumikia wananchi wa Jiji hili na inaonyesha tumekuja hapa
kufanya mchezo wa kuigiza” alisema
Aliongeza kuwa kufatia wajumbe ambao ni waheshimiwa
madiwani kwa umoja wao na kwa masilahi ya wananchi ambao wanawawakilisha kuamua
kuweka tofauti zao za kisiasa na kuungana kuikataa rasimu hii kujadiliwa
kutokana na kutokidhi ni vyema mkajipanga kuanda na kurekebisha kasoro hizo ili
kujadiliwa kuletwa na kuwasilishwa ili kuwapa mwanya wa kujadiliwa.
Meya Mabula aliahilisha kikao hicho kwa kumtaka
Mkurugenzi Alfa Hassan Hida kuitisha kikao cha dharula cha Kamati ya Fedha
(FINENCE) kesho asubuhi majira ya saa 3:00 na mchana majira ya 6:00 kuwe na
kikao cha dharula kuipitia baada ya kufanyiwa marekebisho kwenye ukusanyaji wa
mapato,kujiandaa kulipa madeni ya wakandarasi utekelezwaji wa miradi katika
sekta za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu ya Barabara kupitia fedha za Mapato ya
ndani. mengineyo.
Kufatia hatua hiyo baadhi ya wananchi wamempongeza
Meya Mabula,Wabunge na waheshimiwa Madiwani kwa kuungana pamoja na kuweka
tofauti zao za kisiasa (Vyama vyao) ili kuhakikisha Bajeti watakayopitisha inakuwa
suluhisho kwa wananchi wa Jiji hili na mwarobaini kwa wanohujumu mapato ya
Halmashauri ya Jiji kupitia vyanzo vyake vya ndani.
“Huyu ndiye Meya, wananchi wa Jiji hili tunaona
amekuwa ni mtu asiyetaka sifa na amekuwa mtu wa kuchukua maamuzi sahihi na kusikiliza
kilio cha wananchi kwani hali ya miundombinu kwa sasa huko kwenye mitaa na kata
inatisha, madeni ya malipo ya fidia ya maeneo yaliyochukuliwa na Jiji ni muda
sasa na huduma za Jamii zinazorota, tunaomba Kamanda awabane kweli kweli”
walisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.