ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 9, 2014

OXFAM YAWEKEZA MAISHA PLUS MSHINDI ZAIDI YA MILIONI 25 KUSHINDANIWA: MWANZA YAANZA KUCHUKUWA FOMU

Mmoja wa wakurugenzi wa Maisha Plus Tv Kaka Bonda (wa kwanza kushoto) amesema kuwa mwaka uu kampuni yake imeamua kuetengeneza fomu na  kuzigawa bure bila malipoTanzania nzima ambapo kwa washiriki wa Maisha Plus ni wale wenye umri wa miaka 21 -  26 na kwa Mama Shujaa ni wale wenye umri wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Mambo yote kesho katika viwanja vya wazi Buhongwa, mtu yoyote anaye jiamini anakaribishwa kushiriki haijalishi unaelimu gani suala ni jeh! una uwezo wa kushiriki shughuli za maendeleo na uzalishaji mali?
Katika mwendelezo wa Kampeni ya Grow unao lenga kumkwamua mwanamke kutoka katika lindi la umasikini, sanjari na kukabiliana na changamoto ya upungufuwa chakula inayolikabili taifa letu, Shirika la Kimataifa la Oxfam na wadau wake limeandaa shindano la Mama Shujaa wa Chakula ikiwa ni msimu wa Tatu litakalousiswa ndani ya kipindi cha kijamii cha Maisha Plus.

Kwa mujibu wa wa Meneja Kampeni ya Haki na Uchumi wa Oxfam Bi. Eluka Kibona amesema kuwa shirika lake liliamua kuwekeza mpango wake ndani ya kipindi cha Maisha Plus ili kuendesha kampeni yake kwa manufaa zaidi kutokana na ubunifu na elimu inayozalishwa ndani ya kipindi hicho ambayo inahitaji kupanuka zaidi kwa wawekezaji kuwekeza kwenye mchezo wa kipindi hicho cha manufaa kwa jamii.
Mkamiti Mgawe Afisa Uchumi na Uchochezi wa Oxfam amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizo fanywa zinaonyesha asilimia 60 ya wanawake Tanzania wananjihusisha na kilimo lakini ni asilimia 3 tu ya wanawake wanaomiliki ardhi, na zaidi ya asilimia 33 ya wanawake hufanyiwa ukatili wa jinsia.

Hivyo shindano la Mama shujaa linalenga kuwahamasisha, kuwawezesha na kuwasaidia wanawake na vijana katika sekta ya uzalishaji wa chakula. Hii ni kwasababu wanawake huzalisha zaidi ya asilimia 70 ya chakula chote kinachozalishwa nchini, ila kwa  bahati mbaya wanawake hao na watoto ndio wamekuwa waathirika wakubwa wa kwanza wa majanga ya njaa na utapiamlo. 
Khadija Liganga toka KIVULINI.
Naye Afisa Habari wa Kivulini Khadija Liganga amewahamasisha wadau wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kesho katika viwanja vya Buhongwa jijini Mwanza kushuhudia yatakayojiri ikiwa ni pamoja na utoaji elimu ambapo mwisho wa siku fursa itakuwepo kwa watakao hitaji kushiriki kuchukua fomu zinazotolewa bure.
Wadau wa habari pamoja na waelimishaji kupitia sanaa nao walikuwepo kwenye mkutano wa utoaji taarifa.
Sekta muhimu habari.
Afisa Uchumi wa Uchochezi wa Oxfam Mkamiti Mgawe (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kushoto ni mmoja wa Wakurugenzi wa Maisha Plus Kaka Bonda na kulia ni meneja Kampeni ya Haki na Uchumi wa Oxfam Bi. Eluka Kibona.
Shughuli ikiendelea.
Point zikinaswa.
Wadau waliojitokeza leo kuchukuwa fomu mkoani Mwanza, wakijaza vielelezo muhimu kushiriki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.