Ubomoaji utatekelezwa na idara ya Mipango miji ya jiji la Mwanza eneo linalojulikana kama city park Garden, vile vile inadaiwa kwamba eneo hilo limekuwa likijengwa vibanda bila kibali cha ofisi ya Mipango Miji huku ikidaiwa ni kinyume cha sheria ya ujenzi ya mipango miji.
Habari kutoka ndani ya ofisi za jiji la Mwanza zimedai kuwa eneo hilo linaweza kubomolewa wakati wowote ili kupisha ujenzi wa uwekezaji mkubwa wa majengo kama yale ya NSSF na PPF yaliyopo katikati ya jiji la Mwanza.
Eneo hilo ambalo pia hujulikana 'KWA WAMBURA' limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya halmashauri ya jiji na mfanyabiashara huyo ambapo kesi ya kumiliki eneo hilo ilifikishwa mahakamani na Bwana Wambura akashinda kesi hiyo.
Inadaiwa kwamba baada ya Wambura kushinda kesi hiyo, alipewa kibali cha kulitunza eneo hilo kutokana na masharti kwamba atengeneze michoro ya kuwekeza kwenye eneo hilo, ambayo itapitishwa na Mipango miji ya jiji la Mwanza.
Hoja iliibuka hivi majuzi ndani ya kikao cha madiwani ambapo jibu kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira bw. Richard Rukambura lilisema kuwa mfanya biashara huyo alishapewa masharti ya kupeleka michoro akashindwa na haijulikani kinachoendelea.
Nae bw. Wambura amesema kuwa yeye aliandaa michoro ya majengo, lakini uongozi wa jiji ukakataa mchoro aliouandaa kwa madai kuwa haufai, hivyo akawaomba wamsaidie kuchora mchoro wanaotaka wao wakakataa bila kutoa ufafanuzi, ndipo naye akaamua kukaa kimya akisubiri kuitwa au kupewa maelekezo toka uongozi huo wa jiji.
Imedaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itakumba hadi maeneo jirani anayofanyia biashara Wambura kwani yanatambulika kuwa eti ni bustani ya jiji na majirani hao hawana hati miliki ya eneo hilo kama ilivyo kwa Wambura.
Swali jingine: Hatma ya Hospitali ya mwananchi na kituo cha polisi ndani ya eneo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.