
Kusherehekea siku ya wapendanao duniani trh 14feb2012 Club Villa Park imeamua kumleta msanii Kidumu kutoka nchini Burundi kama zawadi kwa wateja wake atakaye burudisha sambamba na bendi ya Super Kamanyola.

Uhusiano wetu na tukio hili ni kuhakikisha wapendanao wanatimiza jukumu la kuhakikisha usalama wao kwa kutumia ipasavyo salama kondom kuepuka maambukizi ya virusi vya ukimwi, magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa kwa wale ambao tafsiri yao ya siku hii huitafsiri vibaya.

Zawadi ni kama kawa Tiketi ya ndege kwa wawili wapendanao kwenda na kurudi Mwanza-Dar kupitia Precision Air.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.