ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 13, 2023

TUNAWAAMBIA WATANZANIA WASITUMIE PODA YA JOHNSON &JOHNSON KWA SASA’- MKURUGENZI WA TBS


Shirika la Viwango nchini Tanzania(TBS) limewataka Watanzania kuacha kutumia poda ya Johnson & Johnson hadi uchunguzi kuhusu poda hiyo utakapokamilika.

Juma lililopita ilifahamika kuwa Shirika la viwango Tanzania, linachunguza poda aina ya Johnson inayouzwa katika maduka mbalimbali nchini humo na kwingineko duniani.

Uchunguzi huo unatokana na kampuni inayotengeneza bidhaa hiyo, Johnson & Johnson ya Marekani kukubali kulipa fidia ya dola za Marekani bilioni 8.9 kwa sababu ya kesi zaidi ya elfu 38 za madai kuwa madini ya talcum yaliyomo kwenye poda hiyo ya watoto na bidhaa nyingine yanasababisha saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi kwa watumiaji.

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athumani Yusuph Ngenya amesema

Poda hiyo ina madhara ambayo yamepigwa marufuku.

‘’Kitu chochea kinachozungumzwa kwamba kina madhara ni bora na ni busara kukiweka kando mpaka uchunguzi ukamilike’’ , alisema na kusisitiza kuwa:’’Tunawaambia Watanzania wasitumie poda ya Johnson & Johnson’’ iliyopo madukani hadi uchunguzi utakapokamilika.

Bw Dkt. Athumani Yusuph Ngenya, amesema uchunguzi kuhusiana na poda ya Jojnson &Johnson ambayo kwa sasa ipo madukani, nchini humo utakamilika katika kipindi cha wiki mbili au wiki tatu zijazo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.