NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Kabla ya Simba Sc kukutana uso kwa uso dhidi ya watani wao Yanga Sc katika Kariakoo Derby pale jijini Dar es salaam, upande wa pili jijini Mwanza mashabiki wa timu hizo ambao ni wafanyakazi kutoka Idara ya Maji safi na Maji taka Mwanza (MWAUWASA) wanasema wao ndiyo wenye funguo za utabiri kwa matokeo ya mchezo huo watakutana katika mchezo uatakaopigwa viwanja vya TTC Butimba wilayani Nyamagana jijini Mwanza. Mchezo huo wa kirafiki wa mashabiki wa Simba na Yanga Idara ya maji safi na maji taka jijini Mwanza utachezwa Jumamosi hii ya tarehe 15 April 2023 majira ya saa 3 kamili asubuhi.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.