TAKRIBANI heka 1,600 za mashamba ya mpunga Kata ya Kagu, Halmashauri ya Wilaya ya Geita mkoani hapa, zipo hatarini kushambuliwa na ndege aina ya kweleakwelea.
Ofisa Kilimo wa Halmashauri, Malick Athuman amesema tayari
mawasiliano na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatirifu (TPHPA) yamefanyika, ili
kuwadhibiti ndege hao ambao idadi yao inaonekana kuongezeka katika eneo hilo.
Amewahakikishia wakulima kwamba changamoto hiyo itaisha, kwa
uendelevu wa zao hilo la chakula na biashara.
Pamoja na kuwathibiti
kweleakwelea shambani, mamlaka itapulizia dawa kwenye mazalia yao kwa kutumia
helikopta, ili kuangamiza kabisa chimbuko lao,
Amedai kuwa kawaida ndege hawa huvutiwa na mazao mengi, ikiwemo
alizeti, lakini wamegundua wanapendelea zaidi mpunga kiasi kwamba wanaweza
kuhama haraka kutoka shamba moja kufuata jingine.Kuwadhibiti ni lazima kwa
sababu wanafanya uharibifu mkubwa kwa kuanza kushambulia mmea wenyewe, hadi
pale mpunga unapoelekea kukomaa.
Ilifahamika
zaidi kwamba kweleakwelea wana uwezo wa kuharibu shamba zima kwa asilimia 100,
kiasi cha mkulima kutopata hata punje ya mavuno.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.