MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Na Oscar Assenga aliyekuwa KILIMANJARO
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amesema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa ubunifu mkubwa alioufanya kupitia Filamu yake ya Royal Tour na matunda yake kuonekana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kuhamasisha utaliiwa ndani ambapo alisema kwamba baada ya ziara hiyo watalii wanaoingia kwa mwaka sasa wameongezeka na kufikia zaidi ya 7000.
Alisema kwamba huo ni ubinifu wa kipekee ambao umefanywa na Mkuu huyo wa nchi katika kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii hapa nchini ikiwa ni kuhamasisha watanzania na w ageni kutoka nje kutembelea hifadhi zilizopo hapa nchini.
Mkuu huyo wa wilaya alisema pia Rais Dkt Samia Suluhu kupitia fedha za Tozo na Fedha za Covid 19 zimewasaidia kuimarisha miundombinu ya hifadhi nchini ambapo miongoni mwa hifadhi ambazo zimenufaika ni mkomazi ambapo kuna majengo ya utawala na barabara nzuri ambao zinahamasisha watalii hivyo Rais amekuwa mfano nzuri wa uhifadhi nchini.
Aidha pia alisema wanapokuwa na hifadhi inayofikika kirahisi wanapata watalii wengi ambazo wanasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu
Hata hivyo aliwahimiza watanzania kutembelea hifadhi za hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo kuwataka pia wananchi wa wilaya ya Same watumie wikiendi zao kuweza kufika mkomazi kuweza kuona vivutio vilivyopo na hivyo kusaidia serikali kuingiza mapato ambayo yatasaidia maendeleo kwenye wilaya yao.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kupelekea fedha za Uviko ambapo waliweza kuzitumia kujenga lango maalumu ambalo ni la kuingilia wageni wanaofika kutembelea hifadhi hiyo na kuweza kupata huduma nzuri za utalii.
Alisema kwamba kupitia fedha hizo wameweza kujenga barabara nzuri yenye utefiu wa zaidia ya kilomita 140 na pia kutengeneza viwanja vya ndege na hiyo imetoa fursa kwa wageni ambao hawana muda wa kutembea kwenye magari kwa muda mrefu wakati wa safari zao kutoka maeneo mbalimbali kwenda kuitembelea hifadhi hiyo
Happiness alisema kwa kujengwa uwanja huo kumesaidia wageni kusafiri kutumia ndege kufika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi moja kwa moja kutoka kwenye viwanja vyengine
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.