Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philipo Isdor Mpango akiwasalimu wananchi wa eneo la Buswelu wilayani Ilemela jijini Mwanza. |
#April 12, 2023 Jumatano
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala pamoja na mkurugenzi wa manispaa hiyo Mhandisi Modest Apolinary wamewaongoza wananchi wa wilaya ya Ilemela katika mapokezi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philipo Isdor Mpango alipofanya ziara katika wilaya ya Ilemela na kuzungumza na wananchi katika eneo la Buswelu senta.
Mkutano ambao pia umehudhuriwa na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe Adam Malima, Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso, Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mhe Deogratius Ndejembi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe Sixbert Reuben na Mbunge wa Jimbo hilo ambae pia ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula (MNEC) ambapo Mhe Dkt Mpango alipata wasaa wa kuhutubia wananchi sanjari na kuelezea shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan, kusikiliza kero zinazokabili wananchi na kisha kuzipatia ufumbuzi
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe Sixbert Reuben.
Mbunge wa Jimbo hilo ambae pia ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula (MNEC)
Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mhe Deogratius Ndejembi.
Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso.
' Ilemela ni yetu, tushirikishane kuijenga '
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.