NA ALBERT GSENGO/MWANZA
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso amewataka wakala wa Majengo Tanzania TBA kuwa na ubunifu katika ujenzi wa majengo mazuri na yenye mvuto wa kibiashara ili wawe na uwezo mkubwa wa kukusanya kipato chao binafsi na kuacha kuitegemea serikali. Kakoso amesema hayo alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la kupangisha lililopo eneo la Ghana wilayani Ilemela jijini Mwanza na kuongeza kwa kumwagiza waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa kuhakikisha anawasaidia TBA waweze kukusanya madeni ambayo wanaidai serikali kupitia taaisisi zake. Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TBA Daud Kondoro amesema ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 50 ambapo amesema wao kama TBA waliona Jiji la mwanza lina uhitajia mkubwa wa Majengo ya kupangisha hivyo ni wajibu wao kuyaendeleza maeneo yote nchi nzima. #samiasuluhuhassan #jembefm #mwanzaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.