Kazi ya kuandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kupitia mfumo wa Biometrick Voters Registration (BVR), ambao huhusisha uchukuaji wa alama za vidole na picha, jana iliingia siku ya tatu, huku baadhi yao wakipongeza utendaji wake.
Kwa mujibu wa ripoti iliyokusanywa na mwandishi wetu inasema kuwa tokea siku ya kwanza lilipoanza zoezi hilo lilionyesha matumaini maana wananchi wetu walijitokeza kwa wingi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi katika vituo vya uandikishaji, wananchi hao walisema kuna mabadiliko ukilinganisha na siku zilizopita, hivi sasa kazi zinafanywa haraka.
“Watu wanaokwenda kwenye vituo kujiandikisha idadi yao ni kubwa kuliko hata makadirio ya tume, kama hawataongeza muda au vifaa, siku saba walizopanga, hazitatosha na wengi wataachwa bila ya kujiandikisha,” alisema.
Baadhi ya waandikishaji na wasimamizi wa mashine wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuongeza muda ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi zaidi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushpoto) , Naibu Katibu Mkuu na Katibu Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzinua Uborereshaji wa Daftarila Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandiskishaji wapiga kura baada ya ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako.
Baadhi ya watalaamu wa kuandikisha wapiga wakiwa na zana za kazi kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzindua Uborereshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.