MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewaagiza wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanalivalia njuga suala la mauaji ya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi “Albino’ kwa kuimarisha ulinzi na usalama usiku na mchana kwa lengo la kuweza kuwabaini wale wote wanahusika na matukio hayo.
Agizo hilo la Injinia ndikilo amelitoa kwa masikitiko makubwa wakati wa sherehe za kuwakaribisha wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni pamoja na kuwakabidhi vitendea kazi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu katika Wilaya zao.
Ndikilo amesema kwamba kwa sasa wimbi la mauaji ya kikatili dhidi ya albino yanazdi kushika kasi katika maeneo mbali mbali ya nchi,pamoja na uvamizi wa vituo vya polisi hivyo kunahitajika nguvu ya ziada katika kuimarsiha ulinzi na usalama ili kuweza kuwepo kwa hali ya amani na utulivu.
BOFYA PLAY MSIKILIZE RC NDIKILO.
Aidha Ndikilo katika hatua nyingine amewataka wakuu hao wa wilaya kwa kushirikina na viongozi wengine kujipanga kikamilifu katika kulitafutua ufumbuzi suala la migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Pwani kwan limeonekana kuwa ni changamoto kubwa ambayo inasababisha hali ya vurugu kwa wananchi wenyewe hususa wakulima na wafugaji.
MSIKILIZE NDIKILO.
Kwa upande wake Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alikuwa na haya ya kusema kuhusina na maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa pamoja na mikakati yake katika kupambana na changamoto hizo.
MSIKILIZE MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO.
WAKUU wa Wilaya ambao wamebadilishwa kutoka maeneo mengine na kupelekwa katika Mkoa wa Pani ni pamoja na pamoja na Subira Mgalu ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Majid Mwanga Bagamoyo,Abdlah Kiato Wilaya ya Mkuranga pamoja na Dr Nassor Amid Wilaya ya Mafia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.