Wafanyakazi wa Airtel wachangia kuboresha mazingara ya shule ya msingi Ushindi
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa “AirtelTunakujali” wakishirikiana na wafanyakazi wa kitengo cha Airtel Biashara za Mashirika wameendeleza dhamira ya kusaidia jamii kwa kukarabati darasa la chekechea katika shule ya msingi Ushindi iliyopo jijini Dar Es Salaam.
Airtel imeendelea kushirikiana na wafanya kazi wake kutoa mchango kwa jamii kwa kuhakikisha shule zinakuwa na miundombinu na mazingira bora ya kujifunza hali itakayochochea wanafunzi kupenda shule.
Uchakavu wa miundombinu ya shule hasa za msingi nchini ikiwemo vyumba vya madarasa ni moja ya chanzo kikuu kinachodhoofisha mahudhurio ya wanafunzi na hivyo kusababisha matokeo yasiyoridhisha.
Mwishoni mwa wiki wafanyakazi wa kitengo hicho walishiriki ukarabati wa darasa hilo la chekechea katika shule ya msingi Ushindi lenye kuhitaji marekebisho makubwa ambayo yanatazamiwa kuongeza hamasa ya watoto kuhudhuria shuleni.
Akizungumza katika tukio hilo mwalimu Mkuu wa Shule ya hiyo Bw Iddi Kaminja alisema, "tumekuwa na changamoto kubwa mahudhurio kutokana na wanafunzi kutokufurahia kuja shuleni na hii inasababishwa na shule kuwa na miundombinu chakavu isiyowapa ari ya kusoma."
"Tangu mpango huu wa ukarabati ulipotangazwa wanafunzi wamekuwa na shauku kubwa ya kutaka zoezi hili liweze kuisha na kuanza kutumia darasa hili. Hali hii limekuwa faraja kwetu hivyo ni wazi kwamba itatusaidia kuongeza kiwango cha mahudhurio shuleni na hatimaye kuongeza kiwango cha elimu hapa shuleni."
Aliongeza Mwalimu Kaminja Aidha Mwalimu Kaminja ametumia fursa hiyo kuwapongeza wafanayakazi wa Airtel kwa moyo wao wa kujitolea kwa hali na mali kuinua kiwango cha elimu ya awali na kutoa rai kwa makampuni mengine kuona umuhimu wa kuborosha madarasa ya shule za awali na msingi kwani njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ni kuwapa watoto wetu mazingira mazuri na yenye usalama wawapo hapo shuleni.
Nae meneja wa Airtel wa huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema,"madarasa mazuri ni muhimu kwa usalama wa wanafunzi lakini pia huleta hamasa ya mahudhurio hivyo ni lazima wazazi wawe tayari kusaidia hatua za haraka kufanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuepusha hatari na gharama kubwa ya fedha. Kwa njia hiyo madarasa haya yatadumu."
"Leo tumeshiriki zoezi hili katika shule ya msingi ya Ushindi lakini kazi hii imekuwa ikifanyika sehemu mbali mbali nchini kupitia mradi wa “Airtel Tunakujali” ambao unawawezesha wafanyakazi wa Airtel nchi nzima kushiriki katika shughuli za kijamii hususan zinazoinua sekta ya elimu
Tunajisikia furaha kuwekeza katika jamii kwa kiwango ambacho kinaleta tofauti kubwa. Siku zote tumelenga kufikisha huduma bora na za gharama nafuu kwa watanzania huku tukitambua na kupambana na changamoto mbalimbali za jamii inayotuzunguka Leo nanyi mnashuhudia utofauti wetu na makampuni mengine, Airtel sio tu inaongoza katika mtandao ulio bora hapa nchini bali pia namna tunavyojali wanaotuzunguka" aliongeza Bayumi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.