Na Victor Masangu, Pwani
WANAFUNZI wa shule ya msingi ya mailimoja iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa baadhi yao wamelazimika kusomea chini ya miti kutokana na madarasa ambayo walikuwa wanayatumia kuezuliwa mabati na kubomoko kutoka na mvua na upepo mkali uliotokea hivi karibuni.
Hali hiyo imebainika baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvester Koka alipofanya ziara maalumu ya kwenda kuitembelea shule ili na kujionea uharibifu mkubwa wa madarasa ambao umejitokeza.
Akizungumza kuhusiana na maafa waliyoyapata Mkuu msaidizi wa Shule hiyo Theresia Mtoni amesema kwamba kwa sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na madarasa 11 kuharika hivyo kuwalazimu wanafunzi zaidi ya 450 kusomea chini ya miti hali ambayo ni hatari kwa usalama wao kwani mazingira wanayosomea sio rafiki.
Mkuu huyo aliongeza kuwa wameamua kutokana na hali hiyo wanafunzi wanasoma kwa zamu ambapo baadhi yao wakiwa wanasoma madarasani wengine wanakuwa wanasomea nje chini ya miti.
“Kwa kweli ndugu mwandishi nadhani wewe mwenyewe umeweza kushuudia hali yenyewe ilivyo tupo katika wakati mgumu sana, kwani vyumba vya madarasa vimeharibika sana nah ii kutokana na upepo mkali uliokuja hivyo kuharibu miundombinu ya madarasa kwa ali halisi ndio hiyo,” alisema Mkuu huyo.
Aidha Mwalimu huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvester Koka kwa kuweza kuonyesha ushirikiana wake wa dhati na kuwasaidia msaada wa mabai 50 pamoja na mifuko ya simenti.
Kwa upande wao wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo iliyokumbwa na maafa hayo akiwemo Diana Mbowe, pamoja na Upendo Chilale walisema kwamba kitendo hicho cha kusomea chini ya miti kinawapa shida kubwa sana kwani hawawezi kusoma kwa uhuru kama ilivyokuwa hapo awali.
Walisema kuwa mbali na kuwepo kwa changamoto hiyo ya kuharibika kwa madarasa pia wanakabiliwa na changamoto nyingine ya kutokuwa na matundu ya vyoo vya kutosha ukilinganisha na idadi ya wanafuzni waliopo na kwamba vilivyopo vipo katika hali ambayo sio nzuri kwani miundombinu yake ni mibovu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvester Koka ambaye alikwenda kutembelea shule hiyo na kuchangia msaada wa mifuko 50 ya simenti pamoja na mabati 50,alisema kwamba atahakikisha kwamba anafanya jitihada za hali na mali ili kuweza kuhakikisha wanafunzi hao wanarejea madarasani na kuendelea na masomo kama kawaida.
Pia Mbunge huyo aliwaomba wazazi kuwa mstari wa mbele katika kuchangia kitu chochote ili kuweza kukarabati miundombinu hiyo ya madarasa lengo ikiwa ni kuunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu katika halmashauri ya mji wa Kibaha na wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.
SHULE ya msingi ya maili moja Wilayani Kibaha ambayo ina wanafunzi 963 kwa sasa inakabiliwa na ubovu mkubwa wa majengo yake ambayo miundombinu yake imeharikika kutokana na upepo ulioambatana na mvua hali ambayo imesababisha wanafunzi kusoma wakiwa chini ya miti.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.