NA PETER FABIAN, MWANZA.
WACHIMBAJI wadogo wa Madini waliojiunga katika vikundi na kupata leseni za uchimbaji madini wametakiwa kufika katika Ofisi za Kanda ili kupewa taratibu wa kuomba mikopo ya fedha za ruzuku zilizotolewa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishina Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa, David Mlabwa jana Ofisini kwake jijini Mwanza, alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini tayari imetenga kiasi cha Sh bilioni tisa ikiwa ni ruzuku kwa ajili ya kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini nchini.
“Wachimbaji waliojiunga katika vikundi na kupewa leseni za uchimbaji wafike katika ofisi zetu za Kanda jijini Mwanza, Geita na Kagera ili kupewa utaratibu utakaowawezesha kujaza fomu maalumu za mkopo kabla ya kupewa mikopo kutafanyika mchujo kuona vikundi vilivyokidhi sifa za uombaji kulingana na taratibu zilizopo,”alisema.
Mlabwa alisema kuwa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na madini anayeshughulikia Madini, Charles Kitwanga “Mawe matatu” wakati akiwa katika ziara ya kutembelea jimboni kwake na kuzungumza na wananchi na wachimbaji katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwagimagi na Mwamala Kata ya Ilujamate wilayani Misungwi aliagiza tuwape utaratibu wa kuomba leseni na walio na vikundi tayari waombe mikopo ya fedha.
“Naibu Waziri Kitwanga alisema wachimbaji wadogo walio kwenye vikundi na tayari wamepewa leseni za uchimbaji mdogo wa madini tuwapatie utaratibu wa kuomba mikopo ili kuwasaidia kupata mitaji ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuchimba kwa vyenzo za Teknolojia kwenye maeneo,”alisema.
Aidha aliongeza kuwa Naibu Waziri, Kitwanga aliagiza kuwa katika maeneo ya uchimbaji ya kijiji cha Ishokelahela Kata ya Ilujamate wilayani Misungwi kuna tatizo linalolalamikiwa na wachimbaji wagodo kukosa maeneo ya uchimbaji na ameelekeza kukaa nao kuona jinsi ya kuwagawia maeneo ili kuwawezesha kuchimba kwa utaratibu wa kufuata sheria ya madini ya mwaka 2010 .
Kamishina Msaidizi Mlabwa alisema kuwa Wizara ya Nishati na Madini imeisha towa maelekezo juu ya wachimbaji wadogo katika maeneo yenye migogoro ili Ofsini za Kanda kukaa na wachimbaji wadogo kuwashirikisha kupitia viongozi wa serikali za vijiji, Kata na Wilaya ili kuwapatia maeneo ya uchimbaji kwa taratibu na sheria.
Wito wangu kwa wachimbaji wadogo katika maeneo waliyopewa kuchimba ni kufuata taratibu na sheria za uchimbaji kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira na kushirikiana kwa kuanzisha, kujiunga katika vikundi vya uchimbaji ili kuomba leseni na kupewa mikopo itakayowezesha kuwa wachimbaji wanaochimba kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.