ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 9, 2025

SALUM MWALIMU AJA NA MAMBO MATATU YA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA NCHINI

Salumu Mwalimu
Mgombea urais wa Chama Cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu,

Mgombea urais wa Chama Cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu, ametaja mambo matatu ambayo atayafanya kumaliza tatizo la ajira nchini.

Mojawapo amesema ni kuboreshe sekta ya kilimo kwa kuifungamanisha na viwanda.

Amesema kilimo kisichofungamanishwa na viwanda ni kilimo mfu na hakiwezi kuwa na faida kwa nchi.

Mwalimu ametoa kauli hiyo Kigamboni, wakati akiendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuaminiwa kuwa rais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwezi huu.

Amesema ili nchi itatue tatizo la ajira ni lazima itengeneze fursa ambazo zinaigharimu kidogo lakini zenye faida kubwa.

"Duniani kote, nchi zinafungamanisha kilimo na viwanda kwa sababu kilimo msingi wake ni kuzalisha malighafi za viwandani.

"Kwa hiyo, Tanzania tusipoheshimu kilimo, hatuwezi kuondokana na tatizo la ajira hata tufanyeje,"amesema Mwalimu.

Jambo la pili ambalo amesema serikali yake italitumia kutengeneza fursa za ajira ni kuboresha mfumo wa elimu ambao utawaandaa Watanzania kupambana na fursa za ajira ndani na nje ya Tanzania.

"Vijana kutoka nchi nyingine, wanakuja Tanzania wanaingia kwenye makampuni yetu na kuchukua ajira zetu kwa sababu vijana wetu uwezo wao wa kufanya kazi katika makampuni hayo ni mdogo kwa sababu elimu yetu haikuwaandaa vizuri.

"Tutaboresha elimu yetu ili kuwaandaa vijana kuziona fursa za ajira na kuwa na uwezo nazo ndani na nje ya Tanzania,"amesema Mwalimu.

Jambo la tatu, amesema serikali yake itahakikisha inazilinda biashara zinazoanzishwa na wananchi wake kuanzia mdogo, za kati na kubwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment