Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo akipandishwa kwenye gari ya Polisi Baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. |
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akipokea taarifa ya shughuli zinazofanywa na Mgodi huo. |
Mganga Mkuu wa Mgodi ambaye pia anasimamia kitengo cha mazingira Mgodini wa Dhahabu wa Geita(GGM)akitoa taarifa ya namna ambavyo mgodi umekuwa ukihifadhi mazingira. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitazama baadhi ya nyaraka wakati ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. |
Moja kati ya Nyumba ambayo hipo ndani ya eneo la Mgodi. |
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akikagua madarasa ambayo yanaonekana kuharibiwa na mipasuko. |
Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo
amekamatwa na serikali baada ya kukutwa na nyaraka za serikali .
Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na
mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata
sheria ya mazingira .
Mhe. Lugola akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Geita ameagiza kukamatwa kwa
mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) David Nzogila baada ya kukutwa na
nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi ya wakala wa utafiti wa jiolojia
Tanzania(GST).
Hata hivyo katika hali hisiyo ya kawaida na bila kutarajia mwanasheria huyo aliyekuwa
akiukingia kifua mgodi huo ili
usikumbane na rungu la fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria
inavyotamka alijikuta akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai
haijaeleza iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi
huo usibebeshwe mzigo huo.
Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe riporti
hiyo ili ajiridhishe lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka
kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake
kuipata Serikalini lakini yeye hawezi
kutoa nyaraka ya serikali, jambo
lililomkasirisha Naibu Waziri wa
Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.
Diwani wa kata ya mtakuja Constatine Morandi ameelezea
kuwa wananchi wamekuwa wakisumbuliwa muda mrefu na mgodi bila ya kupatiwa fidia
na kwamba kutokana na wao kuwa ndani ya
bikoni kumesababisha kutokupatiwa huduma mbali mbali za kijamii hivyo ni vyema kwa serikali wakaweka nguvu
kuwasaidia wananchi hao.
Bw Abdallah Omary-Mkazi Nyamalembo alimweleza
Naibu waziri kwamba wamekuwa wakiishi
maisha ya mashaka kutokana na hali ilivyo ya maeneo hayo ya mgodini na kwamba
mgodi ulikwisha wai kuwapatia fidia ya shilingi elfu ishirini jambo ambalo
limeonekana kuwa ni udhalilishaji kwani pesa hiyo ni ndogo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa mgodi huo Saimon Shayo,alisema kuwa eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilalamika
kuhusu suala la fidia hadi sasa kuna nyumba mbili na kwamba fidia ya kwanza
walilipa kiasi cha sh,Bilion Moja na waliipatia serikali iweze kuwafidia
wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.