ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 21, 2013

TEMBEZA MACHO NA PICHA ZA UDIFERENTI SOKO LA KIMATAIFA KIRUMBA MWALONI

Ile unaingia tu katika soko la Kimataifa la samaki Mwaloni Kirumba jijini Mwanza pembeni kushoto langoni kuna wachuuzi wa kuni lakini sikujua zinakotoka.

Mitumbwi hii licha ya kufanya shughuli za uvuvi pia husafiri kuelekea visiwa mbalimbali vilivyoko ndani ya ziwa Victoria ambavyo vina maelfu ya watu waishio humo wenye mahitaji kwaajili ya kupeleka bidhaa mbalimbali za matumizi ya kila siku.

Magugu maji kando kando mwa mwalo huu ulio pembezoni mwa ziwa.

Wa mazingira mpooo..? 

Zao la ndizi limeshamiri kweli sokoni hapa.

MitumbwizZ...

Nyanya area...

Bidhaa zisaririshwazo kwaajili ya ujenzi.

Sekta ya dagaa...

Dagaa ni bidhaa inayosukuma kwa asilimia kubwa uchumi wa wakazi wa Mwanza hivyo wafanyabiashara wengi huwa bize wakishughulika mkono kwa mkono kuhakikisha shughuli zinasonga.

Mlima Dagaa, kufika kileleni dakika sifuri.

Mzigo full packed tayari kwa biashara kubwa.

Kila kukicha malori ya uzito mbalimbali huingia sokoni hapa na kutoka na shehena za kutoka za bidhaa za samaki kwaajili ya soko la Afrika Mashariki na Kati. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.