ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 9, 2024

KILA ABIRIA ATAKAYEPANDA NDEGE UTAPANDWA MTI JIJINI MWANZA NA VIA AVIATION


 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

Utafiti umebaini kuwa viumbehai wa kuvutia kama ndege, mimea na wanyama siku moja wanaweza kufutika katika uso wa dunia kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa na binadamu ambao hivi sasa umeleta mabadiliko ya tabia nchi. Wataalam wanasema mabadiliko ya tabianchi yanatokana na tabia ya watu kukata miti hovyo na kuiacha ardhi ikiwa uchi hivyo kuongeza hewa chafu ya ukaa angani ambayo uzalishwa na viwanda, vyombo vya usafiri nchi kavu, majini na angani pamoja na uchomaji taka hivyo kuleta athari kubwa kwa viumbehai wote ambao wanakuwa katika hatari ya kutoweka katika uso wa Dunia. Kwa kuliona hilo wadau wa maendeleo taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa huduma mbalimbali za ndege VIA AVIATION Mwanza inakuja na kampeni ya 'MTI MMOJA KWA KILA HUDUMA' yaani kila mteja atakaye kata tiketi ya ndege kupitia wakala ya kampuni hiyo basi utapandwa mti kwaajili ya kutunza mazingira

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.