ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 21, 2012

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI KUANZA KESHO MUSOMA


Na. Shommy Binda
Mashindano makubwa ya ngoma za asili ambayo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa kudhaminiwa na kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Balimi yatafanyika kesho kwa upande wa Mkoa wa Mara katika ukumbi wa bwalo la Mageraza huku jumla ya vikundi vikitarajiwa kushiriki mashindano hayo.

Akizungumza na Mwandishi wa blogu hii hii leo Mjini Musoma meneja wa TBL Mkoa wa Mara Polycalipo Makunja,amesema taratibu zote kuhusiana na mashindano hayo ikiwemo kuwasiliana na vikundi vyote kutoka katika wilaya zote za Mkoa wa Mara zimekwisha kamilika kilichobakia ni kuona ni kikundi gani kinaibuka washindi hapo kesho na kwenda kuuwakilisha mkoa wa Mara katika mashindano ya kanda yatakayofanyika Julai 28 Jijini Mwanza.

Poly amesema awali mashindano hayo yalikuwa yafanyike jumamosi Julai 21 lakini wameamua kuyasogeza mbele kwa siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kutangaza siku tatu za maombolezo kufuatia ajali ya meli ya MV Karama kuzama katika bahari ya Hindi ikiwa njiani kuelekea visiwani Zanzibar.

Amesema vikundi 10 kati ya 12 vilivyojitokeza kushiriki mashindano hayo vitakuwa na nafasi ya kupata zawadi kutokana na maandalizi mazuri ambayo yameboleshwa kwa mashindano ya mwaka huu.

Meneja huyo wa TBL Mkoa wa Mara amesema mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ataondoka na kitita cha shilingi laki sita,shindi wa pili laki tano,mshindi wa tatu laki nne na mshindi wa nne shilingi laki tatu.

Ameongeza kuwa kuanzia mshindi wa tano hadi wa kumi kila mmoja ataondoka na kifuta jasho cha shilingi laki moja na nusu huku burudani mbalimbali zikitarajiwa kusindikiza mashindano hayo.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda wa kampuni ya TBL Andrew Mbwambo amesema mashindano ya ngoma za asili ya Mwaka huu yanatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na vikundi kupewa maandalizi ya muda mrefu na kuongezeka kwa zawadi za washindi.

Mbwambo ameongeza kusema kuwa kutakuwa hakuna kiingilio chochote katika kushuhudia mashindano hayo hivyo kila mmoja anaruhusiwa kwenda kushuhudia katika ukumbi wa bwalo la magerza mjni Musoma ni ngoma gani ya asili ya Mkoa wa Mara itakayoibuka kidedea na kwenda kuwakilisha katika mashindano ya kanda jijini Mwanza julai 28.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.