ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 14, 2019

WAGANDA 800 WASAINI WARAKA WA KUTAKA KUFIKISHWA ICC RAIS MUSEVENI.


Waganda 800 wasaini waraka wa kutaka kufikishwa ICC Rais Museveni
Zaidi ya wananchi 800 wa Uganda wamesaini waraka wa kushinikiza kufikishwa katika Mahakama ya Kimataia ya Jinai ICC, Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.
Kampeni hiyo inayokusudia kukusanya kwa akali saini milioni mbili inaongozwa na kinara wa upinzani nchini humo Dakta Kizza Besigye, ambaye alikuwa mkuu wa chama cha  Forum for Democratic Party (FDC).
Iwapo watafanikiwa kukusanya sahihi hizo, watawasilisha waraka huo kwa mwendesha mashitaka wa ICC, ili kuanzisha mchakato wa kufunguliwa faili la jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu dhidi ya Museveni katika mahakama hiyo iliyoko mjini The Hague nchini Uholanzi.
Baadhi ya ushahidi dhidi ya Museveni ambao wapinzani wanategemea kwenye kesi hiyo, ni mauaji ya watu 100 wakati maafisa usalama walipovamia makazi ya mfalme wa kitamaduni, Omusinga Charles Wesley Mumbere katika mji wa Kasese miezi kadhaa iliyopita.
Dkt Besigye akibebwa hobelahobela na maafisa wa polisi Kampala
Wapinzani nchini Uganda wanalalamika na kuituhumu serikali ya Rais Yoweri Kaguta Museveni kwamba, imekuwa ikiendesha siasa za mkono wa chuma dhidi ya mrengo wa upinzani, hatua ambayo wanaitaja kuwa, inakandamiza na kubinya demokrasia katika nchi hiyo.
Rais Museveni ambaye amekuwa akiongoza Uganda tangu mwaka 1986 anatazamiwa kuwania tena kiti hicho mwaka 2021 na kuendelea hadi mwaka 2026, baada ya bunge la nchi hiyo kufuta kipengee cha sheria juu ya ukomo wa umri wa kugombea urais nchini humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.