WANDISHI toka vyombo mbalimbali vya habari mkoani Mwanza wamejumuishwa kwenye moja ya kamati muhimu katika maandalizi ya sherehe za Uhuru 2019.
Wakiongozwa na Ally Nyakia ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba wanahabari waliowekwa kwenye kamati ya Burudani Uhamasishaji Habari na Matangazo ni pamoja na Mabere Makubi wa ITV, Team yote ya Shirika la Habari na Utangazaji Tanzania (TBC) tawi la Mwanza, Albert G. Sengo wa Jembe Fm na Gsengo Blog pamoja na George Binagi wa MBG Habari.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye ndiye aliyekuwa akiziainisha kamati hizo amesema kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ameelekeza sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika (Disemba 9) mwaka huu 2019 kufanyika kitaifa mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo kabla kutatanguliwa na shughuli mbalimbali za kijamii kwa viongozi kushiriki mkono kwa mkono shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile kufungua miradi, utengenezaji matofali, kujenga madarasa, kushiriki shughuli mbalimbali mashambani (hasa ikizingatiwa kwamba huu ni msimu wa kilimo) makongamano na kadhalika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.