Habari kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania zinasema kuwa Chama cha Wananchi (CUF) hatimaye kimejitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.
Kimesema kuwa kimejitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato huo ikiwa ni pamoja na kuenguliwa asilimia 90 ya wagombea wake.
Msimamo huo umetangazwa leo Jumanne na Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati akitoa maazimio ya kikao cha baraza kuu la uongozi la CUF. CUF kinakuwa chama cha siasa cha sita kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini Tanzania baada ya Chadema, ACT- Wazalendo, NCCR –Mageuzi, UPDP na Chauma.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.