TANZANIA imepanda Kwa nafasi 22 kwenye viwango vya FIFA duniani kutoka
nafasi ya 157 kwa mwezi wa pili na sasa imeshika namba135. Hii inatokana
na Stars kufanya vizuri kwenye mechi mbili za kirafiki dhidi ya
Botswana waliyoshida kwa magoli 2-0 na Burundi iliyoshinda kwa magoli
2-1.
Pia Brazil imeipiku Argentina kwenye nafasi ya kwanza kwa mwezi wa tatu
Argentina ilikuwa nafasi ya kwanza kwa mwezi wa pili huku Brazil wakiwa
nafasi ya pili. Haya ndio mataifa kumi yanayoongoza kwenye viwango vya
soka Duniani 1. Brazil 2. Argentina 3. Germany 4. Chile 5. Colombia 6.
Ufaransa 7. Ubeligiji 8. Ureno 9. Uswisi na 10. Hispania.
Mataifa 10 yanayongoza Afrika, kwenye mabano ni nafasi zao za viwango vya ubora duniani.
1. Misri (19) 2. Senegal (30) 3.C ameroon (33) 4. Burkinafaso (35) 5.
Nigeria (40) 6. DR Congo (41) 7. Tunisia (42) 8. Ghana (45) 9. Ivory
Coast (48) 10. Morocco (53)
Kwa Afrika Mashariki Uganda inaendelea kuongoza ikiwa nafasi 72 ikiwa
imepanda nafasi 3 kutoka 75 ya mwezi wa Pili, Kenya nafasi 78 nayo ikiwa
imepanda Kwa nafasi 10 kutoka 88 ya Mwezi uliopita wakati Rwanda
yenyewe inakamata nafasi ya 117 ikiwa imeshuka kwa nafasi 17 kutoka
nafasi ya 100 ya mwezi uliopita na Burundi ambao ilifungwa na Tanzania
ipo katika nafasi ya 141 nayo ikiwa imeporomoka kwa nafasi 3 kutoka
nafasi ya 138 ya mwezi wa pili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.