UGC Katika notisi, karani wa Bunge la Kitaifa Serah Kioko alifahamisha wabunge hao kwamba ziara ya utambulisho itafanika leo na kesho.
Vikao elekezi vitajumuisha usajili wa Wanachama, ukusanyaji wa taarifa za bio-data, utoaji wa vitambulisho vya ubunge, kutoa taarifa kuhusu matumizi ya mfumo wa upigaji kura bungeni.
Katibu wa Bunge alisema kuwa itahusisha pia ziara ya Majengo ya Bunge na maelezo mafupi ya Ofisi ya Karani kuhusu mambo muhimu ya kisheria, pamoja na mambo mengine.
Kioko alidokeza kuwa Wabunge Wateule watafahamishwa mara tu Rais Uhuru Kenyatta atakapotangaza tarehe watakayokutana kwa kikao cha kwanza.
Watatembezwa kwenye Majengo ya Bunge na pia watapewa taarifa pamoja na mambo mengine huduma na vifaa vinavyopatikana kwa ajili ya Wajumbe.
Wabunge wapya pia watawezeshwa kujiandikisha kwa huduma na vifaa ikiwa ni pamoja na bima ya matibabu na huduma zingine zinazohusiana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.