ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 24, 2022

FCC YAWAPIGA MSASA WADAU WA KAHAWA MKOANI KAGERA

NA ALBERT G.SENGO. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila ametoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Kagera kubaini vikundi au makundi yanayojihusisha na uzalishaji mali vinavyohudumiwa na Serikali ili kulinda bidhaa ya Mtumiaji wa kahawa. Mhe. Albert Chalamila ametoa maelekezo hayo wakati akifungua semina ya masuala ya Ushindani na Udhibiti wa bidhaa bandia kwa wadau wa Sekta ya Kahawa Mkoani Kagera, Semina hiyo iliyoandaliwa na FCC imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera ikivijumuisha vyama vya ushirika vya vya wakulima na wazalishaji wa zao Kahawa Wilayani Karagwe na Mkoani Kagera (KDCU na KCU) ikiwa ni pamoja na wakulima, wazalishaji na wadau wa zao hilo kwa ujumla. " Tunazungumzia kahawa ya hapa kwetu Kagera yenye ubora mzuri lakini michakato ya kuivuna na maandalizi ya kupata zao lenyewe bado inatumia mchakato wa kizamani na kufanya watumiaji kuacha kahawa yetu na kutumia kahawa nyingine" amesema Mhe. Chalamila.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.