NA ALBERT G. SENGO
Kirumba ni moja ya kata zenye mishemishe na pilika pilika nyingi jijini Mwanza.
Mbali ya kuwa na soko kubwa la Kimataifa la Biashara ya Samaki lililopo Mwaloni, pia katika kata hiyo kuna jengo kubwa la kisasa la biashara lenye maduka ya huduma mbalimbali kubwa na ndogo ndogo nazungumzia Rock City Mall, ambapo humo ndimo kuna ile bar maarufu ya burudani na vyakula vya kitalii The Cask Bar and Grill.
Uwanja maarufu Afrika Mashariki uliochukuwa jina la kata hiyo (Kirumba Stadium) unapatikana Kirumba.
Kata ya Kirumba pia ni maarufu kwa huduma za Gesti, Hotels na chocho za mengineyo yanayowafanya watu kukesha.
SENSA iliyoanza usiku wa saa 6:01 kuamkia Tarehe 23 imegusa vipi maeneo hayo...?
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.