NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini kimewataka viongozi wa CCM kuanzia katika ngazi za Kata, Wilaya na Mkoa kutoingilia kabisa maamuzi ya wana ccm pamoja na wananchi katika suala zima la kuwachagua viongozi wanaowapenda katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu kwani wao ndio wanawafahamu vizuri uwezo wao wa kuchapa kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) mwalimu Mwajuma Nyamka wakati wa kikao cha Halmashauri kuu CCM Wilaya ya Kibaha mji ambacho kimefanyika kwa lengo la kuweza kupitisha utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka 2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na chma.
Nyamka amebaainisha kwamba lengo kubwa la chama cha mapinduzi ni kuhakikisha inaweza kushinda kwa kishindo katika mitaa yote hivyo ni wajibu wa viongozi wote wa CCM kuanzia ngazi za mashina na matawi kushikama kwa pamoja na kwamba kutokana na kazi nzuri ambayo imefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika miradi mbali mbali ya maendeleo watatembea kifua mbele katika kuomba kura kwa wananchi.
Kadhalika Mwenyekiti huyo aliwapongeza madiwani wa Halmashauri ya mji Kibaha pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega katika suala zima la utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwa sambamba na kutatua kero na changamoto za wananchi.
"Pamoja na juhudi kubwa ambazo zinafanywa na CCM kusimamia utekelezaji wa Ilani lakini bado kuna baadhi ya watendaji wa mitaa,na kata wamekuwa ni kama tatizo kubwa kwa wananchi kiasi cha kupelekea kuwakwaza kwa kiasi kikubwa kutokana na kutoa lugha zisizokuwa na staha kabisa na kwamba hawataweza kuwawafumbia macho hata kidogo watendaji wa namna hiyo kwani watatupunguzia kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa,"alisema Nyamka.
Pia katika Katika kikao hicho Mwenyekiti Nyamka amesema kwamba wameiagiza Halmashauri ya mji Kibaha kuhakikisha kwamba wanaitunza miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo imemalizika hususan katika miundombinu ya barabara.
"Tumepitisha utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu wa 2024, lakini kitu kikubwa tumeagiza halmashauri yetu ya mji kuitunza miundombinu ya barabara hasa katika maeneo yenye lami kwani kumukuwa na changamoto ya kutozitunza maana utakuta maeneo mengine nusu kifusi cha mchanga na nusu lami,"alibainisha Nyamka.
Aidha Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kuna baadhi ya halmashauri nyingine wameweka mikakati ya kuzitunza barabara zao kwa kuzifanyia usafi na kuzifagia lakini kwa upande wa Halmashauri ya kibaha mjini jambo hilo linakuwa ni vigumu hivyo linapaswa kufanyiwa utekelezaji.
Pia Mwalimu Nyamka amesema kwamba kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara ambao unafanywa na baadhi ya madereva kupitisha magari ya mchanga yenye uziti mkubwa ambayo ndio yamekuwa ni moja ya chanzo cha kufanya barabara ziweze kuharibika kwa haraka.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji Issack Kalleiya ametumia kikao hicho kutoa pongezi kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji Kibaha kwa kuweza kubuni vyanzo vipya amabvyo vimepelekea kuongeza zaidi ukusanyaji wa kasi ya kuongeza mapato.
Kadhalika Katibu kalleiya amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, madiwani,pamoja na Mbunge kwa kuweza kushikamana kwa pamoja katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amemshukuru na kumpongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi katika Halmasshauri ya mji wa Kibaha ambazo zimeweza kuleta matokeo chanya katika suala zima la kuwasaidia wananchi katika miradi mbali mbali za maendeleo.
Aidha Mkuu huyo alisema kwamba kwa ushirikiano mkubwa ambao anaupata kutoka kwa viongiozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Madiwani wote pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini,mkurugenzi wameweza kutekeleza Ilani ya chama kwa kiwango kikubwa ikiwemo kumsaidia Rais katika utekelezaji wa majukumu yake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.