ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 10, 2014

WASHTAKIWA KUSOTA LUMANDE

Watuhumiwa wa Kuchakakachua bidhaa za kampuni mbalimbali wakisindikiwa mahakamani kujibu tuhuma zao leo mida hii katika mahakama ya mjini Moshi Tanzania. (Picha kwa hisani ya prhabari.blogspot.com)






Moshi

WATUMIWA SUGU WA KUCHAKACHUA VIROBA VYA KONYAGI WASHINDWA DHAMANA NA KURUDISHWA RUMANDE.

WAELEZEWA NI WATU HATARI SANA WAIOFAA KUACHILIWA KWA DHAMAN

WANATUHUMA KILA PEMBE YA NCHI IKIWEMO DAR ES SALAAM

YAELEZWA, KONYAGI FEKI WANAZOTENGENEZA ZIMEATHIRI WATANZANIA WENGI 

BAADHI YA WAMILIKI WA MABAA WALIOHUDHURIA MAHAKAMANI HAPO WAMETOA RAI KWA WANANCHI KUACHA KUNUNUA KONYAGI VICHOCHORONI NA BADALA YAKE KWENYE MABAA HALALI AU MADUKANI


MAHAKAMA ya hakimu mkazi Moshi, leo imefurika mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia watuhumiwa sugu wa utengenezaji wa konyagi feki na bidhaa nyingine mbalimbali na kuzibandika nembo za TRA ambayo inadiwa kudhuru maelfu ya watanzania.

Hata hivyo mahakama ya mkazi moshi imewaachia kwa dhamana watuhumiwa hao nane ambao wanakabiliwa na tuhuma za kutumia alama za biashara za makampuni mengine kwa nia ya kutapeli.na kujipatia pesa kinyume cha utaratibu.

Watuhumiwa hao ni Yusuph George, Richard Leonard, Preygod Urassa, Mohamed Rashid, Greyson Jonathan, George Kisivani, Hagai Nelson na Jackson Shayo, ambao wanatuhumiwa kwa pamoja kwa
kutumia kwa nia ya kutapeli alama ya biashara ya Konyagi kinyume cha sheria huku wakijua wazi ya kuwa alama hiyo ni ya kibiashara ya halali ya kampuni ya Tanzania Distilleries Limited.

Watuhumiwa hawa wana kesi mbalimbali ikiwemo ile ya kutumia nyaraka za mamlaka ya mapato nchini TRA ikiwemo mihuri yenye namba za kodi ya mapato jambo ambalo linadaiwa kuikosesha serikali mapato mengi.

Wakili wa serikali Julius Semali ameiambia mahakama ya mkazi Moshi kuwa watuhumiwa hao ni hatari na kwamba wanakabiliwa na kesi za namna hiyo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Singida wana kesi ya namna hii na ambayo itaendelea tena Aprili   30, 2014, Ilala wanatafutwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka za TRA wakati Arusha wanatafutwa kwa kukiuka dhamana na kutoroka mwaka 2012.

Pamoja na kupewa dhamana kwenye kesi hiyo huko Moshi, bado hakimu aliamuru warudishwe rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Kesi hii imevutia wammia ya wakazi ambapo miongoni mwao ambao ni wafanyabiashara za mabaa wametoa wito kwa wananchi kuepuka kunywa konyagi vichochoroni kutokana na madhara ambayo wameshapata watu wengi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.