ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 11, 2014

MABONDIA MIYEYUSHO, CHEKA, KING CLASS MAWE WAPIMA UZITO KUPAMBANA JUMAMO.

Bondia Mustafa Dotto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'KIng class Mawe' kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi katikati ni Promota Jay Msangi. 
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mustafa Doto utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam.
Bondia Sukkasem Kietyongyuth kushoto akiwa na kocha wake Win Panyaparichot wakati wa upimaji uzito
Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi. 
Bondia Sukkasem kietyongyuth kutoka Tahiland akituishiana misuli na Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi. 
Bondia Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba kushoto ni bondia Gavad Zohrehvand wa Iran.

Baadhi ya waandishi wa habari na taswira yao kikazi zaidi.

Na Mwandishi Wetu
 Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi' Mawe naBondia SukkasemKietyongyuth  kutoka Thailand wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi ya April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba

Mpambano huo wa raundi kumi utasindikizwa na mabondia Fransic Cheka na bondia Gavad Zohrehvand wa Iran atakayecheza raundi 8, mbali na mapambano hayo kutakuwa na mpambano mwingine utakao wakutanisha mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atakaye pambana na Mustafa Doto mpambano wa Raundi sita.


Pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi yatakayo sindikiza mchezo huo katika ukumbi wa PAT Sabasaba Dar es salaam ambapo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile:- Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Chachu zaidi ni kwamba kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.