ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 11, 2014

BILIONEA WARREN BUFFET AMWAGA MABILIONI KUPAMBANA NA UJANGILI TANZANIA.

BILIONEA namba tatu duniani Warren Buffet, ametoa misaada mbalimbali kwa Wizara ya Maliasili na Utalii yenye thamani ya bilioni nane kwa ajili ya kupambana na ujangili katika mbuga pamoja na mapori ya akiba.
Bilionea Buffet ametangaza ufadhili wake huo wakati akizungumza katika hafla maalumu iliyofanyika katika Chuo cha Taaluma cha Wanyamapori cha Pasiansi, kilichopo Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu.
  
Msaada wa  bilionea huyo kupitia taasisi yake ya Warren G Buffet ni pamoja na ununuzi wa Helkopta mbili aina ya R44,ambazo zitakamilika katika kipindi cha miezi sita pamoja na mafunzo kwa marubani wanne,kugharimia wataalamu elekezi,magari matano aina ya Landcruiser.

Tajiri huyo raia wa Marekani pia amegharimia ukodishaji wa Helkopta ambayo tayari imeanza kazi katika pori la Selou,wakati ikisubiri kukamilika kwa utengenezaji wa Helkopta mpya mbili ambazo zimeaagizwa toka nchini Marekani.

Bilionea Buffet pia amegharimia uhifadhi na utafiti wa duma katika hifadhi ya Serengeti na kutoa kiasi cha shilingi bilioni 2.2.

Taasisi nyingine ambayo imenufaika na ufadhili wa bilionea huyo ni Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi ambao watajengewa mabweni sita yenye thamani ya shilingi bilioni 2,282,000/= kwa ajili ya wanachuo 300.

Chuo hicho pia kitanufaika kwa kununuliwa mabasi mawili yenye thamani ya shilingi milioni  490,960,000/=,malori mawili aina ya Scania yenye thamani ya shilingi milioni 240,590,000/=,darubini 24 zenye thamani ya shilingi milioni 24.

Naye Waziri Nyalandu alisema kuwa Wizara yake imejipanga kikamilifu kupambana na ujangili kw adhati na kawme haitaweza kurudi nyuma kwa suala lolote lile hadi pale itakapotokomeza ujangili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.