TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA
MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 14.03.2018
¨ WATU NANE (08) WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI WILAYANI
NYAMAGANA.
KWAMBA
TAREHE 13.03.2018 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI KATIKA MTAA WA MABATINI KUSINI
KATA YA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU NANE
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.DEUS LUCAS, MIAKA 52, DIWANI WA KATA YA MABATINI
- CHADEMA, 2. DANIEL MONGO, MIAKA 46, MWENYEKITI CHADEMA TAWI LA KILOLELI B”, 3.
LAURENCE CHILO, MIAKA 21, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MTAA WA MABATINI, 4.LAMECK
KAUNDA, MIAKA 38, MKAZI WA KILOLELI B, 5.JACKSON MADEBE, MIAKA 44, MKAZI WA
MTAA WA MWANANCHI, 6.BI SECILIA BUTUKO, MIAKA 4O, MKAZI WA MTAA BUGARIKA,
7.MWITA SAGALI, MIAKA 38, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA NA 8.SELEMAN GABRIEL, MIAKA
45, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA
KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI
POLISI WALIPOKEA TAARIFA TOKA KWA WASIRI KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU LIPO
KUNDI LA WATU KATI YA 200 NA 500, WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
WAMEKUSANYIKA KATIKA NYUMBA ALIPOPANGA BWANA LAURENCE CHILO, HUKU WAKIWA
WAMEFUNGA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA SPIKA ZA MATANGAZO. HUKU WANACHAMA HAO WA CHADEMA WAKIDAI KUWA WAMEKWENDA KUMUHANI
MWANACHAMA MWENZAO BWANA LAURENCE CHILO ALIYEPATWA NA MSIBA WA KUFIWA NA MAMA
YAKE MZAZI MIEZI SITA ILIYOPITA KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KISHA
KWENDA KUZIKA NYUMBANI KWAO UTEGI WILAYANI TARIME MKOANI MARA MWAKA JANA.
AIDHA
BADAE ILIDAIWA KUWA JAMBO LILILOKUWA LIKIENDELEA KATIKA KIKAO HICHO NI UGAWAJI
WA KADI ZA CHAMA, KUANDIKISHA WANACHAMA WAPYA NA KUTOA HOTUBA.
ASKARI WALIFIKA
KATIKA ENEO LA TUKIO KISHA KUWAITA VIONGOZI NA KUONGEA NAO ILI KUWEZA KUFAHAMU UHALALI WA KIKAO
HICHO NDIPO GHAFLA WALIANZA KURUSHA MAWE KWA ASKARI. ASKARI WALIWEZA KUJIHAMI
VIZURI KISHA WALIFYATUA MABOMU YA MACHOZI HEWANI KUWATAWANYA NA BAADAE
WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WAFUASI NANE TAJWA HAPO JUU WA CHAMA HICHO.
KATIKA
ENEO LA TUKIO KUMEPATIKANA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, KADI ZA
CHADEMA ZILIZOANDIKWA MAJINA NUSU, KADI ZA CHADEMA AMBAZO HAZIJAANDIKWA MAJINA
NA KADI ZILIZOANDIKWA MAJINA, MIHURI MIWILI, KARATASI TATU ZENYE MAJINA YA
MAHUDHURIO NA T-SHIRT ZENYE NEMBO YA CHADEMA. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA
MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA
MAHAKAMNI. UFATILIAJI WA KUHAKIKISHA MJI UNAKUWA SHWARI UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA ONYO KWA
VIONGOZI WA SIASA NA WANACHAMA WAO KWA UJUMLA AKIWATAKA KUACHA TABIA ZA HOVYO AMBAZO ZIPO KINYUME NA SHERIA NA
TARATIBU ZA NCHI ZENYE LENGO LA KUONDOA UTULIVU KATIKA MKOA WETU. KWANI SUALA
HILO HALIKUBALIKI NA TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WANAOKWENDA KINYUME NA SHERIA ZA
NCHI.
PIA EMEOMBA WANANCHI WAELEWE KUWA AMANI NA UTULIVU NA USALAMA MKOANI
KWENTU NA NCHI YETU KWA UJUMLA NI JAMBO LA MSINGI. BILA UTULIVU, AMANI NA
USALAMA HAKUTAKUWEPO NA SHUGHULI YEYOTE YA MAENDELEO ITAKAYOFANYIKA KWA HIYO
TUEPUKE WALE WOTE WANAOSHAWISHI VURUGU/FUJO. PIA ANAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE
KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA
UHALIFU WA AINA KAMA HII ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA
SHERIA.
IMETOLEWA
NA:
DCP:
AHMED MSANGI
KAMANDA
WA POLISI (M) MWANZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.