![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa km 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 katika eneo la Kigongo, Misungwi mkoani Mwanza tarehe 19 Juni, 2025. Daraja hilo ambalo ni sehemu ya barabara ya Usagara-Sengerema-Geita ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Sirari hadi Mtukula na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi Februari, 2020. |
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipepeza bendera ya taifa kuruhusu mabasi na magari kupita kwenye daraja hilo rasmi badala ya kutumia vivuko. |
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipungia mkono abiria wa gari la kwanza (basi) lililopata idhini ya kufungua safari rasmi kupitia daraja hilo. |
Tupe maoni yako



0 comments:
Post a Comment